IQNA

Uislamu unaenea kwa kasi nchini Zimbabwe

19:20 - May 15, 2017
1
Habari ID: 3470981
TEHRAN (IQNA)-Uislamu unaenea kwa kasi nchini Zimbabwe huku wakaazi wengi wa nchi hiyo wakiwa sasa wanafahamu na kukubali mafundisho ya dini hiyo tukufu.

Kwa mujibu wa Sheikh Shaibu Asali, Mkuu wa Kitengo cha Kiarabu cha Chuo cha Kiislamu Harare, ustawi wa Uislamu Zimbabwe ni kwa ajili ya mazungumzo baina ya dini.

Katika mahojiano na gazeti la Sunda Mail, Sheikh Asali amesema kati ya wakaazi wote milioni 15 Zimbabwe, karibu asilimia tatu ni Waislamu.

Ameongeza kuwa ingawa Waislamu bado ni wachache lakini hivi sasa wameanza kuimarika katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya Wakristo na watu wa dini za jadi.

Amesema miaka ya nyuma ni watu wachache waliokuwa wakiufahamu Uislamu kwani kulikuwa na sera za kuwapinga Waislamu hasa vijijini.

Hatahivyo hali hiyo imebadilika kwani kuna vitabu vingi kuhusu Uislamu ambavyo vimesambazwa kote Zimbabwe. Aidha amesema katiba ya mwaka 2013 ya Zimbabwe iliruhusu uhuru wa kuabudu na hivyo kuondoa ile dhana iliyokuwepo miaka ya nyuma kuwa Uislamu ni dini ya wageni. Sheikh Asali anasema kuna misikiti 20 Harare, misikiti minane Bulawayo na misikiti mingine mingi kote Zimbabwe.

Hivi sasa ni jambo la kawaida kuwaona Wazimbabwe wazalendo wakiwa wamevaa kanzu na kofia wakienda msikitini kwa ajili ya ibada au masomo ya Kiislamu.

Pamoja na hayo, Waislamu Zimbabwe, sawa na maeneo mengine duniani, wangali wanakabiliwa na changamoto za propaganda za vyombo vya habari ambavyo vinaeneza chuki dhidi ya Uislamu na kuinasibisha dini hii tukufu na ugaidi.

Pamoja na hayo kuna nuka chanya ambazo zinashuhudiwa Zimbabwe kama wakati mbunge wa Harare Terence Mukupe aliposema kuna uwezekano wa kushirikiana na Waislamu katika kujenga shule. Mbunge huyo ameonekana kufurahishwa na itikadi ya Waislamu ya kutoa sadaka kwa wasiojiweza katika jamii.

Kwa kuzingatia kuwa Malawi ina idadi kubwa ya Waislamu, hakuna shaka kuwa Uislamu pia utaenea katika maeneo mengine ya kusini mwa Afrika.

3462836
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Rashidkiveukakai.
0
0
Ningetamani Mimi Niwe Wa Kwanza Kuanthini Katika Inji Hio.ash Hadu Alaa Ilaaha Ila Llaah,ash Hadu Anna
محمد لراسوولو لله.
وا على واليىولله.
Na Nifundishe Hata Alif,be,the.Na Watakia Waislamu Wote
صاوم ماقبول.
captcha