IQNA

Kinara wa Chuki dhidi ya Uislamu acheza dansi katika kasri ya mlezi mkuu wa magaidi

0:43 - May 22, 2017
1
Habari ID: 3470990
TEHRAN (IQNA)-Rais Donald Trump wa Marekani katika safari yake ya kwanza ya kigeni ametembelea Saudia kwa madai ya kuunganisha dunia katika vita dhidi ya ugaidi.


Hii ni katika hali ambayo Trump anajulikana kuwa kinara wa chuki dhidi ya Uislamu duniani huku Saudia nayo ikiwa ni mlezi mkuu wa kiroho wa magaidi wakufurishaji duniani ambao wanafuata itikadi ya Kiwahhabi ambayo ni itikadi rasmi Saudi Arabia.

Trump alipata umashuhuri katika kampenzi zake kwa kueneza fikra na mitazamo ya chuki dhidi ya Uislamu na pia baada ya kuchaguliwa alipitisha sheria ya kuwapiga marufuku watu kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kuingia nchini humo. Saudia nayo ni kitovu cha fikra za Kiwahhabi ambazo zinatumiwa na magaidi wa makundi kama vile ISIS, Al Qaeda, Taliban, Boko Haram na Al Shabab.

Mnamo Mei 20, Trump akiwa ameandamana na mke wake waliingia Riyadha kwa ajili ya kikao kilichotajwa kuwa ni cha Uislamu na Marekani mjini Riyadh.

Viongozi wa Saudi Arabia na Marekani wamesaini makubaliano kadhaa katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya kijeshi, yenye thamani ya dola bilioni 380. Aidha mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud amemvisha Trump mkufu wa dhahabu wenye gharama kubwa na kucheza naye mziki wa dansi ya kijahilia.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa Jumamosi, yalitiwa saini mjini Riyadh baina ya Rais Donald Trump wa Marekani na Mfalme wa Saudia, Salman bin Abdulaziz Al Saud. Kufuatia utiaji saini huo, White House imedai kuwa, makubaliano hayo muhimu ya kijeshi baina ya Saudia na Marekani yana lengo la kuiruhusu Washington kutoa ulinzi kwa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi kutokana na hatari ya ugaidi. Kinara wa Chuki dhidi ya Uislamu acheza dansi katika kasri ya mlezi mkuu wa magaidi

Hayo yanajiri katika hali ambayo sehemu kubwa ya silaha zinazonunuliwa na Saudia kutoka Marekani, ndizo zinatumika kuishambulia nchi jirani ya Kiislamu ya Yemen huku sehemu nyingine ya silaha hizo ikigawiwa na Riyadh kwa makundi ya kigaidi yanayotekeleza jinai kubwa nchini Iraq, Yemen na Syria. Safari ya Rais Trump nchini Saudia na ambayo ni ya mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa Marekani nje ya nchi tangu alipochaguliwa kuwa rais, imekosolewa sana na Waislamu duniani hasa kutokana na rais huyo kuwa na chuki kali dhidi ya Uislamu na wafuasi wa dini hii tukufu ya mbinguni.

Katika tathmini jumla kuhusu malengo hasa ya safari ya Trump katika Asia Magharibi au Mashariki ya Kati, tunaweza kusema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Marekani imekuwa ikifuatilia malengo yaliyo na utata mkubwa katika eneo na madamu nchi hiyo itaendelea kufuatilia malengo hayo haramu ni wazi kuwa itaendelea kuitazama Iran, ambayo imesimama imara mbele ya malengo hayo, kuwa ni tishio. Kwa msingi huo tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na rais huyo wa Marekani kuwa Iran inaunga mkono ugaidi si jambo geni.Kinara wa Chuki dhidi ya Uislamu acheza dansi katika kasri ya mlezi mkuu wa magaidi Suala lisilo na shaka ni kuwa Trump ameonyesha kuwa na tamaa na pupa kubwa katika kuingilia masuala ya Mashariki ya Kati lakini kwa kutilia maanani ukosoaji na upinzani mkubwa ambao umekuwa ukimkabili katika ngazi za kimataifa kuhusu misimamo yake isiyo ya kimantiki, bila shaka rais huyo hataweza kubuni muungano imara wa uhasama dhidi ya Iran wala kutoa uungaji mkono wa kutosha kwa watawala wa Saudi Arabia kama wanavyotarajia.

3601610


Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Mohamed omary
0
0
Nafikiri America haitakii mema ulimwengu wa kiislamu huku sisi waislamu wenyewe tikishindwa kutafakari nini lengo la amerika
captcha