IQNA

Waislamu waliokuwa katika ibada waokoa watu wakati wa moto mkubwa London

15:04 - June 15, 2017
Habari ID: 3471019
TEHRAN (IQNA)-Waislamu waliokuwa wameamka kutekeleza ibada za usiku za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani walifanikiwa kuokoa maisha ya watu wengi wakati wa kuanza kuteketea moto jengo la Grenfell Tower mjini London.

Taarifa zinasema wakazi wa jengo hilo wanasema hawakusikia sauti za kengele za mfumo wa kuashiria kuanza kuteketea moto jengo hilo la ghorofa 24 katike eneo la London Magharibi mtaa wa Kesington Kaskazini. Taarifa za kwanza za kuzuka kwa moto jumba hilo ziliripotiwa saa, 00:54 BST Jumatano (saa tisa kasoro dakika tisa alfajiri Afrika Mashariki). Hadi sasa watu 30 wanaripotiwa kupoteza maisha katika mkasa huo. Kikosi cha Zimamoto cha Uingereza kimesema kuwa mashine 45 na maafisa 200 wa Zimamoto pamoja na magari 20 ya wagonjwa yameshiriki katika juhudi za kuzima moto wa jengo hilo lililojengwa mwaka 1974.

Wakazi wengi wanasema Waislamu ndio waliowafahamisha moto umewaka kwani wengi walikuwa macho kwa ajili ibada za usiku na daku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wakazi Waislamu katika jengo hilo waliwagongea milango majirani zao wakiwataka waondoke haraka kutokana na moto uliokuwa ukienea kwa kasi. Gazeti la The Star limewataja Waislamu katika jengo hilo kuwa ni mashujaa wa tukio hilo

Moto huo ulianza dakika chache baada ya saa sita usiku wakati wakazi wengi wasiokuwa Waislamu katika jengo hilo tayari walikuwa wameshalala.

Maafisa wa kuzima moto wanasema Waislamu walikuwa na mchango mkubwa katika kuwasaudia watu kuondoka katika jengo hilo kabla halijateketea kikamilifu na hivyo kupunguza mafa. Aidha Waislamu walio katika mtaa huo wamepongezwa kwa kutoa msaada wa chakula na makazi kwa watu ambao nyumba zao ziliteketea moto.

Wakati huo huo serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May iko chini ya mashinikizo kujieleza baada ya kupuuza uimarishaji wa mbinu za kukabiliana na moto pamoja na kuwepo tahadhari kuwa majengo mengi, kama lililotetekea moto la Grenfell, yanakabiliwa na hatari ya kuteketea. Mkuu wa Ofisi ya May, Gavin Barwell analaumiwa kuwa, wakati wakiwa waziri wa nyumba, alikataa kutoa idhini ya kuimarishwa usalama katika majengo mengi pamoja na kuwa mpango huo uliakhirishw akwa miaka kadhaa. Kiongozi wa Upinzani Uingereza Jeremy Corbyn ametaka wote waliohusika katika kashfa hiyo wawajibishwe.


Waislamu waliokuwa katika ibada waokoa watu wakati wa moto mkubwa  London


Waislamu waliokuwa katika ibada waokoa watu wakati wa moto mkubwa  London

Waislamu waliokuwa katika ibada waokoa watu wakati wa moto mkubwa  London

3463116
captcha