IQNA

Pogba, mchezaji ghali zaidi wa soka duniani azungumza kuhusu imani yake ya Kiislamu

13:56 - July 02, 2017
Habari ID: 3471046
TEHRAN (IQNA)- Paul Pogba, mchezaki soka wa timu ya Manchester United ya Uingereza ni Mwislamu anayefungamana na mafundisho ya dini amesema Uislamu hauna uhusiano na ugaidi.

Pogba ambaye ni mchezaji ghali zaidi wa soka duniani amezungumzia pia kuhusu hali ya Waislamu katika mji wa Manchester nchini Uingereza bada ya hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi ambayo kundi la kigaidi la ISIS lilidai kuhusika nayo.

Pogba anasema alisikitishwa sana na hujuma ya kigaidi ya Mei 22 katika ukumbi wa Manchester Arena ambapo watu 23 walipoteza maisha. Anasema kuwa mashambulizi kama hayo ya kigaidi yanachafua jina la Uislamu. "Ulikuwa wakati mgumu sana, lakini huwezi kupoteza matumaini," alisema. Mchezaji huyo maarufu wa soka anasema huweza ukamuua mwanaadamu asiye na hatia kisha usema umetenda jinai hiyo kwa jina la dini. "Huu si Uislamu na kila mtu anafahamu hilo," ameongeza.

Hivi karibuni pia mchezaji huyo wa kimataifa ambaye ni raia wa Ufaransa alipakia mtandaoni picha yake akiwa katika mji mtakatifu wa Makka kwa ajili ya Ibada ya Umrah na kuandika "kitu cha kupendeza zaidi nilichowahi kukitazama maishani mwangu."Pogba, mchezaji ghali zaidi wa soko duniani azungumza kuhusu imani yake ya Kiislamu

Katika msimu wa Ligi Kuu ya England iliyomalizika mwaka huu, Pogba alifunga mabao 54 na kuiwezesha Manchester kushika nafasi ya sita katika ligi hiyo. Aidha Man U ilitwaa ubingwa wa Ligi ya Europa. Klabu ya Man U ilimnunua Pogba kutoka klabu ya Juventus ya Italia Agosti mwaka jana kwa kitita cha Euro millioni 105 au Pauni za Uingereza millioni 89 na hivyo kumfanya mchezaji huyo kuweka rekodi kama mchezaji ghali zaidi wa soka duniani.

3614439/

captcha