IQNA

Wanajeshi 15,000 Wazayuni wauzingira Msikiti wa Al-Aqsa, Wazuia Sala ya Ijumaa, Wapalestina 4 wauawa

19:03 - July 21, 2017
Habari ID: 3471077
TEHRAN (IQNA)-Wanajeshi 15,000 wa utawala wa Kizayuni wa Israel leo wameuzingira msikiti wa al-Aqsa na kuwazuia Waislamu kuswali Ijumaa huku kukiwa na sheria kali za usalama.

Aidha hadi sasa Wapalestina wanne, akiwemo mtoto aliyekuwa na umri wa miaka 7, wameuawa shahidi katika makabiliano baina wanajeshi wa Israel na Wapalestina wanaolalamikia ukiukwaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa al-Aqsa.

Duru zinasema Wapalestina wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi wa Isael kuwafyatulia risasi za plasitiki Waislamu waliokusanyika nje ya msikiti wa al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, Ismail Haniya amelaani vikali hatua ya Israel ya kuwazuia Waislamu kuingia msikiti wa al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Utawala haramu wa Israel uliwazuia wanaume wote walio chini ya umri wa miaka 50 kuingia katika uwanja wa Msikiti wa al Aqsa. Ijumaa iliyopita Israel pia iliufunga msikiti wa al-Aqsa baada ya oparesheni ya vijana Wapalestina iliyopelekea wanajeshi wawili wa Kizayuni kuangamizwa na Wapalestina watatu kuuawa shahidi.

Wapalestina wadhalilishwa katika upekuzi wa Israel

Utawala wa Israeli uliufungua tena msikiti huo Jumapili na kuweka sheria kali za usalama jambo ambalo limewakasirisha Waislamu ambao wameamua kuswali nje ya msikiti huo kuliko kudhalilishwa na wanajeshi wa Israel kwa jina la upekuzi wa kiusalama.

Idara ya Waqfu katika Msikiti wa al-Aqsa ilitoa wito kwa miskiti yote mjini Quds ifungwe leo Ijumaa ili Waislamu wote mjini humo wakusanyike kuelekea katika Msikiti wa Al Aqsa kulalamikia upekuzi mkali na kamera za usalama za Israel zilizowekwa katika msikiti huo ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu. Kiongozi wa Hamas Ismail Haniya ametoa wito kwa viongozi wa Kiislamu na hasa nchi za Kiarabu kuitisha mkutano wa dharura kujadili namna ya kukabiliana na njama za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqsa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametoa wito wa kuitishwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kwa shabaha ya kujadili njia za kukabiliana na hatua mpya za utawala haramu wa Israel katika mji wa Baitul Muqaddas na Msikiti wa al Aqsa.

Saudia yashirikiana na Israel katika njama dhidi ya al-Aqsa

Katika hali ambayo njama za utawala haramu wa Israel dhidi ya Masjidul-Aqsa zimeshika kasi katika siku za hivi karibuni, habari zinaripoti kuwepo harakati za utawala wa Aal-Saud kwa ajili ya kuiandalia mazingira Israel iweze kuudhibiti kikamilifu msikiti huo.

Miongoni mwa njama zinazofanywa na watawala wa Saudi Arabia dhidi ya msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu duniani, ni kuwashawishi na kuwashinikiza Wapalestina waachane na aina yoyote ya muqawama na mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika uwanja huo Ahmed Bin Saeed al-Qarni, mmoja wa mamufti wakubwa wa Saudia hivi karibuni amenukuliwa akiwataka Wapalestina na Waislamu wa dunia wawaachie msikiti wa al-Aqsa Mayahudi. Mufti huyo wa Saudia amesema wazi katika hotuba yake kwamba, nchi za Kiarabu kamwe hazitotuma jeshi lao kwa ajili ya kuukomboa msikiti huo.

Aidha hadi sasa Wapalestina watatu, akiwemo mtoto, wameuawa shahidi katika makabiliano baina wanajeshi wa Israel na Wapalestina wanaolalamikia ukiukwaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa al-Aqsa.

Duru zinasema Wapalestina wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi wa Isael kuwafyatulia risasi za plasitiki Waislamu waliokusanyika nje ya msikiti wa al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

3621272

captcha