IQNA

Mamia ya Nakala za Qur’ani zasambazwa Puntland, Somalia

19:59 - July 23, 2017
Habari ID: 3471081
TEHRAN (IQNA)-Mamia ya nakala za Qur’ani Tukufu zimesambazwa katika shule moja nchini Somlia miongoni mwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Shirika la Maendeleo Afrika limesembaza nakala hizo hivi karibuni katika eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland nchini Somalia. Nakala hizo za Qur’ani zimekabidhiwa wanafunzi wa shule ya kuhifadhi Qur’ani Puntland katika sherehe zilizohudhuriwa na mkuu wa shirika hilo Yasir Sharmake Othman na Abdurazzaq Umar Farih naibu gavana wa Puntland.

Mkuu wa Shirika la Maendeleo Afrika amesema nakala hizo za Qur’ani zimetolewa na mfadhili kwa msingi wa Sadaqah Jariya kwa lengo la kustawisha na kuimarisha itikadi za kidini nchini humo. Sadaqa Jariya ni sadaha ambayo thawabu zake huendelea kumfikia mwenye kutoa hata baada ya kufa kwake.

Amesema wanalenga pia kuwahimiza wanafunzi wa shule hiyo kuhifadi Qur’ani na pia kufahamu maana ya wanachosoma.

3619850

captcha