IQNA

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

Utawala wa Kizayuni unacheza na moto kwa kukandamiza Wapalestina Quds Tukufu

12:15 - July 24, 2017
Habari ID: 3471082
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba 'unacheza na moto' kutokana na kushadidisha ukandamizaji dhidi ya Wapalestina wa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya Arab League iliyotolewa leo Jumapili naAhmed Aboul Gheit, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo imesema kadhia ya Quds ni mstari mwekundu ambao Waislamu na Waarabu kote uliwenguni katuhawawezi kuiruhusu Israel kuukanyaga.

Sambamba na kuashiria kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu itafanya mkutano wa dharura Jumatano ijayo mjini Cairo Misri kuhusu kadhia ya Quds, taarifa hiyo imesisitiza kuwa, utawala haramu wa Israel unachochea mgogoro mkubwa ambao hauwezi kuuzima kati yake na nchi za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu.

Tangu tarehe 14 Julai mwaka huu, Israel imeshadidisha siasa zake za ukandamizaji dhidi ya Wapalestina katika Msikiti wa al-Aqsa, ambapo hadi sasa Wapalestina watano wameuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Wasiwasi wa Umoja wa Mataifa

Hii ni katika hali ambayo,António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili na hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwazuia Wapalestina kutekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al-Aqsa,katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu wa Quds (Jerusalem).

Huku akiashiria hatua ya kuanzishwa kampeni ya 'Quds ni mpigo wa Moyo wa Intifadha', katika mitandao ya kijamii, Muhammad Abu Tarbush, mkuu wa idara ya maelezo ya Taasisi ya Kimataifa ya Quds amesema kwamba lengo kuu la kampeni hiyo ni kulifanya suala la Quds lizingatiwe kimataifa katika mijadala ya kisiasa na ya vyombo vya habari pamoja na kuyahamasisha mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yaunge mkono kimaanawi na kifedha Beitul Muqaddas. Wimbi la hasira ya Wapalestina na maandamano wanayoyafanya kwa minasaba tofauti dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Israel, yanabainisha wazi kwamba mapambano yao dhidi ya ukandamizaji wa utawala huo ghasibu hayawezi kuzimwa kwa njia yoyote ile bali yanaendelea kuimarika kila siku. Hilo ndilo jambo ambalo limevuruga kabisa mipango na njama zote za utwala huo na hivyo kuufanya uchanganyikiwe usijue la kufanya.

Njama za Israel dhidi ya Masjidul Aqsa

Hatua za kichochezi ambazo zimekuwa zikitekelezwa na askari wa utawala haramu wa Israel huko Masjidul Aqsa, baadhi zimekuwa zikivunjia heshima moja kwa moja matukufu ya Kiislamu na hivyo kuamsha hasira ya Wapalestina na fikra za waliowengu duniani. Hatua za kujipanua utawala huo katika eneo hilo ambalo ni takatifu kwa dini zote za mbinguni, zimeongezeka katika miazi ya hivi karibuni hasa kutokana na uungaji mkono wa viongozi wa Marekani kwa utawala huo. Kwa kuizingira kikamilifu Beitul Muqaddas na kujaribu kubadili muundo wa jamii ya eneo hilo kuwa ya Kizayuni, utawala ghasibu wa Israel unafanya njama za kubadilisha eneo hilo takatifu kuwa mji mkuu wake. Utawala huo unatekeleza njama hizo sambamba na juhudi zake za kujiarifisha mbele ya jamii ya kimataifa kuwa ni dola la Kiyahudi. Beitul Muqaddas ni eneo ambalo linapewa kipaumbele maalumu katika siasa za kibeberu za watawala wa Israel. Lengo la mwisho la utawala wa Israel ima ni kuharibu kabisa Msikiti wa al-Aqsa, kubadilisha utambulisho wake na kuufanya kuwa wa Kizayuni au kuufanya utumike kwa malengo mengine kinyume na ilivyo hivi sasa.

3463443

captcha