IQNA

Warsha ya Waalimu wa Shule za Kiislamu Uganda

12:29 - July 24, 2017
Habari ID: 3471083
TEHRAN (IQNA)-Waalimu wa shule za Kiislamu (Madrassah) nchini Uganda wameshiriki katika warsha ya kuimarisha ujuzi wao.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo imeandaliwa na ofisi ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda katika Madrassha ya ‘Madinatul Ilm’ iliyoko mjini Buwenge mashariki mwa nchi hiyo.

Kati ya maudhui katika warsha hiyo zilikuwa ni ‘sifa za mwalimu wa Kiislamu’, ‘mbinu za kusimamia madrassah’, ‘mbinu za kuamiliana na watoto’, ‘mbinu za kuwafunza watoto’, na ‘utafiti na tathmini’.

Waalimu na wakuu wa shule 50 wa shule za Kiislamu kutoka maeneo mbali mbali ya Uganda walishiriki kwa warsha hiyo.

Aidha Ali Bakhtiari, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda, mhadhiri kutoka Iran, Roshan Zamir, Yusuf Mungir Makanga Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu cha Imam Sadeq AS na Kisigi Abdul mtaalamu wa usimamizi wa taasisi za kielimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala walikuwa miongoni mwa wahadhairi katika warsha hiyo.

Uganda ni nchi iliyo katika eneo la Afrika Mashariki na Waislamu wanakadiriwa kuwa karibu asilimi 20 ya watu wote milioni 40 nchini humo. Uganda pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC.

3622031
captcha