IQNA

Magaidi wa Taliban waua watu 35 nchini Afghanistan

6:29 - July 25, 2017
Habari ID: 3471085
TEHRAN (IQNA)-Kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika na hujuma iliyopelekea watu 35 kuuawa wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa Jumatatu katika shambulio la kigaidi Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.

Mauaji hayo yametokea baada ya gaidi mmoja kujiripua ndani ya gari inayotajwa kuwa ilikuwa imetegwa mada za miripuko magharibi mwa mjiwa Kabul. Polisi ya Afghanistan imesema kuwa, kuna uwezekano idadi ya wahanga wa hujuma hiyo ikaongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa na hali mbaya.

Kwa kuzingatia kuwa eneo la magharibi mwa mji wa Kabul nimakazi yaWaislamu madhehebu ya Shia, inasadikiwa kuwa shambulio hilo limewalenga watu wa jamii hiyo.

Hujuma hiyo imetokea wakati Waislamu wa madhehebu ya Shia wa kabila la Hazara wakikumbuka mwaka moja tokea ijiri hujuma ya kigaidi mjini Kabul ambapo watu 84, wengi wakiwa ni wa jamii hiyo, waliuawa katika hujuma ya kigaidi.

Shambulizi hilo la mjini Kabul linatajwa kuwa kubwa kati ya hujuma nyingizilizoitikisa Afghanistan katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni. Takwimu za Wizara ya Afya nchini humo zinasemakuwa, karibu watu 1700 wameuawa katika wimbi la mashambulizi ya kigaidi ndani ya miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.

Rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai amelaani shambulizi hilo la mjini Kabulna hujuma nyingine za anga za askari wa Marekani katika mkoa wa Nangarharambazo zote zimesababisha mauaji ya makumi ya raia wasio na hatia.

 Ugaidi umekithiri Afghanistan pamoja na kuwepo vikosi vamizi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani katika nchi hiyo na hujuma hizo za kigaidi zinatoa kisingizio kwa wanajeshi hao kuendelea kubakia katika nchi hiyo ya Kiislamu yenye utajiri mkubwa wa madini.

3622385

captcha