IQNA

Waislamu 4 wauawa katika hujuma ndani ya msikiti Cameroon

10:40 - September 14, 2017
Habari ID: 3471172
TEHRAN (IQNA)-Waislamu wameuawa wameuawa baada ya gaidi kujilipua ndani ya msikiti kaskaini mwa Cameroon, ambapo maafisa wa usalama wanashuku kundi la kigaidi la Boko Haram limehusika na hujuma hiyo.

Taarifa zinasema katika hujuma hiyo ya Alhamisi Alfajiri binti aliyekuwa na umri wa miaka 12 au 12 alifika katika msikiti wa Sanda-Wadjiri katika eneo la Kolofata wakati wa adhana ya Alfajiri na kujilipua wakati watu wakiwa wamesujudu. Katika tukio hilo waumini wanne walipoteza maisha na gaidi pia aliangamia katika hujuma hiyo.

Kundi la kigaidi la Boko Haram lenye makao yake Nigeria limekuwa likitekeelza hujuma katika eneo la Ziwa Chad linalojumuisha Nigeria, Cameroon, Niger na Chad. Kundi hilo limekuwa likitumia watoto wadogo kutekeleza hujuma katika miezi ya hivi karibuni.

Tokea Boko Haram ianzishe uasi wake Nigeria mwaka 2009, watu elfu 20 wamepoteza maisha. Aidha zaidi ya watu milioni mbili wamefanywa wakimbizi kufuatia ugaidi wa Boko Haram.

Neno Boko Haram kwa lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.

3641872/4

captcha