IQNA

UN:Utawala wa Kizayuni unaweka vizingiti katika ustawi wa Palestina

10:58 - September 14, 2017
Habari ID: 3471173
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umeulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzuia maendeleo pamoja na kuzorotesha hali ya kibinadamu katika ardhi za Palestina zilizo katika eneo la Quds Mashariki, Ukingo wa Maghribi na Ukanda wa Ghaza katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 ya kukalia kwa mabavu maeneo hayo.

Katika taarifa yake ya Jumanne Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara (UNCTAD), limesema uchumi wa Palestina umedorora kupita kiwango cha wastani.

Ukanda wa Ghaza umekuwa chini ya mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel tokea Juni 2007 na kupelekea kushuka kiwango cha maisha na kuongezeka umasikini katika eneo hilo.

Wakazi milioni mbili Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza hupata umeme kwa muda wa masaa matatu au manne kwa siku huku mzingiro wa Israel ukiendelea katika eneo hilo.

Katika upande mwingine Wazayuni 600,000 wanaishi katika vitongoji 230 haramu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki, maeneo ambayo yanakaliwa kwa mabavu na Israel tokea mwaka 1967.

Wapalestina wanasisitiza kuwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan uwe sehemu ya dola huru la Palestina katika mustakabali huku Quds Mashariki ikiwa mji mkuu wake.

3463900

captcha