IQNA

Kampeni ya kuwasaidia Waislamu wa Myanmar yaanzishwa Kenya

12:58 - September 16, 2017
Habari ID: 3471176
TEHRAN (IQNA)-Msikiti wa Jamia mjini Nairobi, Kenya umezindua kampeni ya kuwasiadia Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaokandamizwa na kuangamizwa kwa umati nchini Myanmar.

Katika taarifa siku ya Ijumaa kuhusu Waislamu hao wa Myamar, Msikiti wa Jamia Nairobi umesema: "Watu wanaokandamizwa zaidi duniani wanakabiliwa na mauaji ya halaiki. Maelfu wameuawa kinyama, wamenajisiwa, wamelazimishwa kuwa wakimbizi na vijiji vyao vimeteketezwa moto. Zaidi ya watu milioni moja wanahitaji makazi, chakula na maji."

Taarifa hiyo imesema, Kamati ya Msikiti wa Jamia Nairobi imezindua kampeni ya mchango wa dharura kwa lengo la kutoa misaada ya kibinadamu kwa Waislamu wa Rohingya.

Msikti wa Jamia Nairobi pia umetoa akaunti maalumu kwa ajili ya kutuma fedha za kuwasaidia Waislamu wa jamii ya Rohingya.

Mauaji yasiyo na huruma ya serikali ya Myanmar kuwalenga Waislamu wa Rohingya yameibua hasira na malalamiko makubwa katika nchi mbalimbali za dunia.Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wameuawa katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na askari wa serikali kwa kushirikiana na Mabudha magaidi. Wimbi jipya la mauaji ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa Myanmar lilianza tarehe 25 Agosti mwaka huu.

3642258

captcha