IQNA

Sayyid Ammar Hakim

Mazungumzo yatumike kutatua mgogoro wa Kurdistan, Iraq

10:54 - September 18, 2017
Habari ID: 3471179
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Ammar Al-Hakim, kiongozi wa Muungano wa Kitaifa, ambao ni mrengo mkubwa zaidi wa kisiasa nchini Iraq amesema kuna haja ya kutumiwa njia ya mazungumzo kutatua hitilafu zilizopo kuhusu eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan nchini humo.

Ameongeza kuwa, mazungumzo ni msingi wa suluhisho katika mgogoro wowote ule. Halikadhalikaametahadharisha juu ya taathira hasi ya kufanyika kura ya maoni ya kujitenga eneo la Kurdistan, akisisitiza kuwa, kitendo hicho hakitakuwa na tija nyingine ghairi ya kuhatarisha usalama, amani na umoja wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Katika hotuba yake ya sala ya Ijumaa, Sayyid al-Hakim alsema hatua ya Serikali ya Kieneo ya Kurdistankushinikiza kufanyika kura ya maoni ya kujitenga eneo hilo na serikali kuu ya Iraq mbali na kuvuruga umoja wa Wairaqi katika kipindi hiki nyeti, pia itaandaa mazingira ya kushuhudiwa mipasuko zaidi na kusambaratika amani na mshikamano wa taifa hilo.

Kauli yaSayyid Ammar Al-Hakim, kiongozi wa Muungano wa Kitaifa nchini Iraq inajiri siku chache baada yaBunge la Iraq kupiga kura kwa kishindo kupinga kufanyika kura ya maoni ya kutaka kujitenga eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Uturuki, serikali kuu ya Iraq na Syria zinapinga vikali wazo la kufanyikakura hiyo ya maoniiliyopangwa kufanyika Septemba 25 mwaka huu.

3643203

captcha