IQNA

Mabuldoza ya Israel yabomoa nyumba za Wapalestina karibu na mji wa Quds

11:45 - September 19, 2017
Habari ID: 3471182
TEHRAN (IQNA)-Jeshi la utawala wa Israel limetumia mabuldoza kubomoa nyumba za Wapalestina katika kijiji kimoja kilichoko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kusini mashariki mwa mji wa Al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo wa Israel.

Katika tukio hilo la Jumatatu, mabuldoza ya jeshi la Israel yalibomoa nyumba katika kijiji cha al Zayyem kwa madai kuwa eti zimejengwa bila vibali.

Wapalestina wanasema kijiji hicho kiko katika kategoria ya Eneo B na liko chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambayo hutoa vibali vya ujenzo na wala si utawala wa Kizayni wa Israel. Bomoa bomoa kawaida hufanyika katika Eneo C ambalo husimamiwa na utawala wa Israel ambao huwanyuma Wapalestina vibali vya ujenzi katika ardhi hizo zao za jadi.

Taarifa ya hivi karibuni ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ilisema Israel imebomoa nyumba 1,089 za Wapalestina mwaka jana hatua ambayo ilipelekea Wapalestina 1,593 kuachwa bila makazi na maisha yaw engine 7,101 kuathiriwa vibaya.

Hayo yanajiri wakati ambao utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kujenga vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zizlizoghusubiwa za Wapalestina.

Hivi karibuni katibu wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema ujenzi na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina umoengezeka kwa asilimia 85 katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu kulinganisha na kipindi kama hicho katika mwaka uliopita.

Saeb Erikat ameeleza kuwa, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu, utawala wa Kizayuni wa Israel umewasilisha mipango isiyopungua 56 ya ujenzi wa nyumba 4,909 katika maeneo ya Wapalestina.

Itakumbukwa kuwa tarehe 23 Desemba mwaka uliopita wa 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio linalotaka kukomeshwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

3463954

captcha