Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo Jumanne mjini Tehran katika kikao na viongozi wa mihimili
mitatu ya dola, yaani vyombo vya mahakama, bunge na serikali kuu.
Sambamba na kuonyesha masikitiko
yake kutokana na ukubwa wa tukio hilo chungu la tetemeko la ardhi
lililoukumba mkoa wa Kermanshah, amelitaja tukio hilo kuwa mtihani wa
Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu ameashiria hatua ya viongozi akiwemo Rais Hassan
Rouhani ya kufika miongoni mwa wahanga wa tukio hilo na kuwapa pole na
matumaini na kussisitiza mshikamano huo katika uga wa utendaji na
kuwasaidia wahanga kwa nguvu zao zote, ili kuweza kuwapunguzia matatizo
yao. Ameashiria hali inayoshuhudiwa ya huruma, mapenzi na kusaidiana
kunakoshuhudiwa katika jamii ya Kiislamu yalivyokuwa na taathira katika
tukio hilo na kusema, tukio hilo la tetemeko la ardhi limewafanya watu
wote kuingia katika ulingo wa kusaidia waathirika na kutaraji kwamba
athari ya mapenzi hayo na udugu na kwa baraka za Mwenyezi Mungu,
zitashamili kati ya wakazi wote wa Kermanshah na kwa taifa lote la Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kubainisha kwamba
Wairan wote wanashirikiana katika msiba huu na watu majasiri na walinda
mpaka shupavu wa mkoa wa Kermanshah, amesema, msiba huu na kuondokewa
watu wao wa karibu ni mchungu sana, lakini anataraji kwamba Mwenyezi
Mungu atashusha utulivu katika mioyo ya watu wa familia zilizoondokewa
na wapenzi wao.
Tetemeko la ardhi lililokuwa la ukubwa wa 7.3 kwa kipimo
cha Rishta lilitokea siku ya Jumapili usiku katika maeneo mbalimbali ya
magharibi mwa Iran na pia katika maeneo ya mashariki mwa Iraq. Hadi
kufikia sasa karibu watu 500 wameaga dunia na wengine, elfu saba
kujeruhiwa katika zilzala hiyo.
3663536