IQNA

Baba amsamehe aliyemuua mwanae kwa sharti kuwa ahifadhi Qur'ani

10:59 - November 16, 2017
Habari ID: 3471265
TEHRAN (IQNA)-Baba nchini Saudi Arabia amemsamehe muuaji wa mwanae kwa sharti kuwa ahifadhi Qur'ani kikamilifu.

Rabi'a al-Dousary, baba yake kijana aliyeuawa ambaye ametambuliwa kwa jina la Abdullah, ameahidi kumsamehe Faisal al-Ameri, mhalifu aliyepatikana na hatia ya kumuua mwanae, kwa sharti la kuhifadhi Qur'ani Tukufu kabla ya kuachiliwa kutoka gereza.

Ameri alihukumiwa kifo kwa kumuua Abdullah al Dousary kufuatia mabishano baina yao mtaani.

Idara ya Gereza katika Mkoa wa Mashariki mwa Saudia imemshawishi Rabi'a al-Dousary amsamehe Ameri.

Aidha amekataa pia kupokea fidia (diyah) au pesa za damu ambazo hutozwa mwenye kuua, na badala yake amesisitiza kuwa Ameria ahifadhi Qur'ani kikamilifu kabla ya kuachiliwa gerezani.

3464430

captcha