IQNA

Indonesia kuzindua Misikiti 1,000 yenye kuzingatia utunzaji mazingira

15:20 - November 18, 2017
Habari ID: 3471268
TEHRAN (IQNA)-Indonesia imetangza mpango wa kuzindia misikiti 1,000 ya 'kijani' kwa maana kuwa kwa maana kuwa ujenzi na utumizi wake umezingatia utunzwaji mazingira.
Indonesia kuzindua Misikiti 1,000 yenye kuzingatia utunzaji mazingiraAkizungumza hivi karibuni, Makamu wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla alisema misikiti hiyo itazinduliwa kabla yam waka 2,000. Ameongeza kuwa katika ujenzi wa misikiti hiyo nukta zitakazozingatiwa na kuwepo nishati jadidika, kuzuia israfu katika utumizi wa maji na pia kuwepo urejelezaji taka (waste recycling) sambamba na kutoa elimu ya kutunza mazingira.

Mradi huo unajumuisha Maulamaa, sekta binafi na idara husika za serikali ambapo kutakuwa na kampeni malumu ya kuwahamasisha Waislamu kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.

"Waislamu wa Indonesia huwasikiliza zaidi maulamaa zaidi ya serikali," amesema Hayu Prabowo mkuu wa idara ya mazingira na mali asili katika Baraza la Maulamaa Indonesia (MUI).

Katika mradi huo misikiti itasaidiwa kuwa na vyanzo vya maji na mbinu za kisasa za kuyahifadhi. Aidha katika upande wa nishati misikiti itahimizwa kutumia nishati ya jua au biogas na hivyo kupunguza gharama za umeme mbali na kutunza mazingira.

Indonesia ni nchi yenye idadi ya watu milioni 250 ambapo karibu asilimi 89 ni Waislamu. Nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira na serikali imechukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.

Kuna misikiti zaidi ya 800,000 kote Indonesia na serikali inatumai kwa kuanza na misikiti 1,000 yenye kuzingatia utunzaji mazingira, mradi huo hatimaye utaweza kuhusisha misikiti yote nchini humo.

3464454

captcha