IQNA

Waziri Mkuu wa Canada apongeza mchango wa Waislamu katika jamii

12:37 - December 24, 2017
Habari ID: 3471322
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa na ni rasilimali muhimu kwa nchi amesema Waziri Mkuu Justin Trudeau katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kuhuisha Uislamu.

"Canada ina bahati kuwa na jamii ya Waislamu wenye harakati," alisema Trudeau katika ujumbe wake maalumu kwa njia ya video.

"Kwa muda wa miaka mingi, Waislamu nchini Canada wameweza kupata ustawi na kutoa mchango mkubwa kwa jamii  huku wakiwa wanadumisha ufungamano muhimu na nchi zao za asili na jambo hilo limewawezesha kuwa na turathi nzuri ya utamaduni."

Waislamu waliwasili Toronto kutoka eneo zima la Amerika Kaskazini kuhuduria kongamano hilo ambalo linafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Toronto Metro.

Pamoja na kuwepo theluji na baridi kali katika mji huo, maelfu ya watu walishiriki katika kongamano hilo la siku mbili.

"Wakati tunakusanyika hapa wikendi hii, tunasherehekea na kutafakari kuhusu anua za jamii jambo ambalo ni chanzo cha nguvu kwa Wacanada," alisema Waziri Mkuu Trudeau.

"Uwepp wa watu wa makabila, dini na rangi mbali mbali ni nukta ambazo zinaifanya jamii ya Canada iwe ya kipekee na iweze kustawi kwa uwazi na kwa kuwajumuisha wote."

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muoongo moja uliopita. Hivi sasa Waisalmu ni asilimia 3.2 ya watu wote milioni 35 nchini Canada.

Waisalmu wamepewa nafasi katika serikali ya Canada na kwa mfani hivi sasa Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia ni Ahmed Hussein ambaye ana asili ya Somalia.

/3675589

captcha