IQNA

Mafunzo kuhusu kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani

22:59 - January 12, 2018
Habari ID: 3471351
TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) lina mpango wa kutoa mafunzo maalumu ya njia za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Mafunzo kuhusu kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu nchini MarekaniOfisi ya CAIR katika jimbo la Washington imeandaa mpang maalumu kwa madhumuni ya kutoa mafunzo kwa raia wa Marekani ya kuwawezesha kuchukua hatua sahihi na athirifu wakati yanapojiri matukio ya vitendo vya chouki dhidi ya Uislamu.

Mafunzo hayo yanatazamiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika mji wa Seattle ambapo raia watapata mafunzo kuhusu jinsi ya kuweza kuchukua hatua athirifu na za usalama wakati yanapojiri matukio na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu.

Zahra Billoo, Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR katika mji wa San Francisco na ambaye pia ni wakili anatazamiwa kuongoza programu hiyo.

Kupitia mpango huo, zinatazamiwa kutolewa taarifa pia kuhusu ongezeko la jinai na uhalifu unaofanywa kwa sababu ya chuki dhidi ya Waislamu na uenezaji hofu na chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani.

Mpango wa  CAIR wa kutoa mafunzo maalumu ya njia za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini humo unatekelezwa katika hali ambayo vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu vimeongezeka mno huko Marekani tangu Donald Trump aliposhika hatamu za uongozi mwaka moja uliopita.

3681100

 

captcha