IQNA

Migogoro ya Ulimwengu wa Kiislamu imetokana na Waislamu kupuuza maamurisho ya Qur'ani

16:06 - June 24, 2018
Habari ID: 3471571
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Iran amesema migogoro katika nchi za Kiislamu inatokana na njama za madola ya kibeberu na pia Waislamu kupuuza maamurisho ya Qur'ani Tukufu kuhusu umoja.

Ayatullah Makarim Shirazi ametoa tamko hilo wakati alipokutana na wanazuoni na wasomi wa vyuo vikuu kutoka Syria Jumamosi huku akisisitiza kuwa nchi za Kiislamu zinahitaji umoja leo zaidi ya wakati wowote ule.

Amesema kuna aya nyingi sana za Qur'ani na Hadithi zinazosisitiza kuhusu umoja. Ayatullah Makarim Shirazi amesema Qur'ani Tukufu imeutaja umoja kuwa ni baraka na kwamba aya za kitabu hicho zinasisitiza kuwa msaada wa Mwenyezi Mungu huwafikia Waislamu walioungana.

Ayatullah Makarim ambaye ni mfasiri wa Qur'ani ameashiria aya ya isemayo «وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِیعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ...Na shikamaneni na Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane (Aal Imran 102)..., na kuongeza kuwa neema za Mwenyezi Mungu huwafikia Waislamu ambao wameungana.

Ayatullah Makarim Shirazi pia amepongeza ushindi wa hivi karibuni wa mrengo wa muqawama au mapambano nchini Syria.

3724695/

captcha