IQNA

Msikiti Mkuu wa Paris

Msikiti Mkuu wa Paris (Grande Mosquée de Paris) ni msikiti mkubwa zaidi nchini Ufaransa. Msikiti huo adhimu ulijengwa kwa usanifumajengo wa Kiislamu baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Msikiti huo ulijengwa kama njia ya kuwashukuru Waislamu waliokuwa katika jeshi la Ufaransa wakati wa vita hivyo. Takribani Waislamu 100,000 waliokuwa katika Jeshi la Ufaransa walipoteza maisha wakiwa wanapigana dhidi ya Wajerumani
Kishikizo: paris