IQNA

Indhari ya AI kuhusu mpango wa Saudia kuwanyonga WaislamuMashia

11:33 - November 09, 2018
Habari ID: 3471735
TEHRAN (IQNA)- Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetahadharisha kuhusu mpango wa utawala wa Saudi Arabia kuwanyonga wafungwa 12 Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithnashariya.

Katika taarifa, Amnesty imesema faili la wafungwa hao sasa limekabidhiwa Idara ya Usalama wa Taifa katika kile kinachoonekana ni hatua ya mwisho kabla ya kutekelezwa hukumu ya kunyongwa.

Vikao vya mahakama Saudia kwa kawida hufanyika kwa siri na bado haijabainika ni lini wafungwa hao walipokabidhiwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Wanaume hao walihukumiwa kunyongwa mwaka 2016 kwa madai bandia ya 'kufanyia Iran ujasusi. Amnesti imesema kesi yao haijafanyika kwa uadilifu. Mwezi Disemba mwaka jana familia za wafungwa  zilifahamishwa kuw Mahakama Kuu ya Saudia imeidhinisha hukumu yao ya kunyongwa na sasa inasubiriwa Mfalme Salman aidhinishe hukumu hiyo. Kwa kawaida iwapo kesi inafikishwa katika Idara ya Usalama humaanisha kuwa hukumu ya kifo inakaribia kutekelezwa. Amnesti inasema kuna Waislamu Mashai 34 ambao wamehukumiwa kifo nchini Saudia, wakiwemo watoto wanne.

3467168

captcha