IQNA

Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani kwa lugha ya Amazigh yazinduliwa

13:33 - January 14, 2019
Habari ID: 3471806
TEHRAN (IQNA)- Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani Tukufu lwa lugha ya Amazigh imezinduliwa nchini Algeria.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Algeria, tafsiri hiyo imeandikwa na  Sheikh Si Hajj Muhnad Tayyib. Katika sherehe za uzinduzi huo mjini Algiers Jumamosi, miongoni mwa waliohudhuria alikuwa ni Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria Mohammad Isa.

Alimpongeza Sheikh Tayyib kwa kazi yake kubwa ambayo ni ya kwanza ya aina yake kwa lugha ya Amazigh.

Tafsiri ya Qur'ani iliyoandikwa na Sheikh Tayyib inajulikana kama  al-Tafsir al- Muyasar Lil-Kalamullah al-Muwaqar na imechapishwa kwa herufi za Kiarabu.  Jumuiya ya Kitaifa ya Maendeleo Endelevu Algeria imesema nakala 100,000 za tafsiri hiyo zimechapishwa na zitasambazwa Algeira na nchi jirani.

Lugha ya Amazigh ni lugha asili ya Afrika Kaskazini na inazungumzwa na watu wa Algeria, Morocco na pia na baadhi ay watu wa Libya, Tunisia, Niger na kaskazini mwa Mali.

3780695

captcha