IQNA

Rais Rouhani wa Iran

Waislamu hawana budi ila kuungana

11:30 - December 27, 2015
Habari ID: 3469883
Duru ya 29 ya mkutano wa Umoja wa Kiislamu imeanza leo hapa mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye amesisitiza kuhusu ulazima wa Waislamu kuungana.

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa viongozi wa nchi za Kiislamu. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Rais Hassan Rouhani amekosoa vikali njama za madola makubwa duniani za kuionyesha dini ya Kiislamu kwamba, ni ya utumiaji mabavu.

Rais Rouhani amesisitiza kwamba, watu wote wanapaswa kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi na makundi yenye misimamo mikali.

Rais wa Iran amekosoa vikali pia hatua ya baadhi ya nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati ya kutumia fedha nyingi kununua silaha na kubainisha kwamba, badala ya kununua silaha fedha hizo zinapaswa kutumika kwa ajili ya kutokomeza umasikini wa kimaada na kiutamaduni baina ya Waislamu.

Rais wa Iran amesisitiza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Kiislamu kwamba, Waislamu hawana chaguo jingine ghairi ya Umoja wa Kiislamu na kwamba, kuna haja ya kuchagua njia sahihi ya kuelekea katika umoja.

Mkutano huo ambao unafanyika kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Wiki ya Umoja wa Kiislamu unahudhuriwa na wageni zaidi ya 300 kutoka nchi 70 duniani. Mkutano wa mwaka huu utajadili mada kuu ya "Migogoro ya Sasa Katika Ulimwengu wa Kiislamu".

Mkutano wa mwaka huu utajadili mada kuu ya "Migogoro ya Sasa Katika Ulimwengu wa Kiislamu" na kwamba kongamano hilo. Mottaki ameongeza kuwa mkutano wa mwaka huu utakuwa na kamati 12 ambazo zitajadili masuala kama vile sayansi na teknolojia, vyuo vikuu, utatuzi wa migogoro, tathmini ya migogoro katika ulimwengu wa Kiislamu na njia za kujikwamua, muqawama, familia, wanawake, biashara na vijana.

3469778

captcha