IQNA

China yapuuza malalmiko na kuendelea kuwakandamiza Waislamu

14:44 - November 13, 2018
Habari ID: 3471740
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa China unaendelea kupuuza malalamiko ya dunia kuhusu kuendelea kuteswa Waislamu waliowachache nchini humo.

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na ripoti kuhusu kukandamizwa na kuteswa Waislamu wa China huku ripoti zikisema zaidi ya Waislamu miliopni moja wa kabila la Uighur wanashikiliwa katika kambi maalumu za mafunzo ya Kikomunisti.

China imepuuza miito ya nchi nyingi duniani ambazo zimeitaka isitishe ukandamizaji wa Waislamu nchini humo lakini wakuu wa Beijing wanadaii hawafanyi kosa lolote.

Mwezi Agosti kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuangamiza Ubaguzi wa Rangi imesema imeandika ripoti kuhusu masaibu ambayo Waislamu wanakumbana nayo katika kambi hizo. Wizara ya mambo ya Nje ya China ilipinga ripoti hiyo kuhusu kukandamizwa Waislamu katika jimbo la Xinjiang. Ripoti hiyo ilisema China inatumia kisingizio cha kukabiliana na ugaidi na misimamo mikali ya kidini kuwakandamiza Waislamu na kuwaweka katika kambi hizo.

Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa inasema, kwa mfano Waislamu wanakandamizwa hata kwa ajili tu ya kutoa salamu za Kiislamu za Assalam Aleikum. Aidha kamati hiyo imesema uchunguzi umebaini kuwa karibu Waislamu milioni moja wa jamii ya Uighur wanashikiliwa katika kambi hiyo.

Mkoa wa Xinjiang una wakazi Waisalmu zaidi ya milioni 10 kutoka kabila la Uighur na katika miaka ya hivi karibuni eneo hilo limeshuhudia makabiliano makali baina ya wanajeshi na Waislamu.

Serikali ya China imechukua hatua kadhaa kuwadhibiti Waislamu katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kumteuwa Mkomunisti mwenye misimamo mikali Chen Quanguo kuwa katibu wa chama tawi la Xinjiang tokea mwaka 2016.

3467213

captcha