IQNA

Sheikh Mohammad Yazbek

Hizbullah itasambaratisha njama dhidi ya Lebanon

12:39 - July 12, 2020
Habari ID: 3472956
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Baraza la Shuraa la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema harakati hiyo inaweza kupambana na kuvunja njama zote za maadui kama tulivyovunja njama zao kijeshi huko nyuma kwa kujiamini na kuwa macho.

Sheikh Mohammad Yazbek amesema hayo na kuongeza kuwa, serikali ya Marekani inabeba dhima ya changamoto, matatizo na shida zote zilizoshuhudiwa huko nyuma na zinazoshuhudiwa hivi sasa katika eneo hili.

Mkuu wa Baraza la Shuraa la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndiyo sababu ya kupata matatizo nchi za eneo hili la Asia Magharibi.

Ameashiria kuhusu matukio yaliyoshuhudiwa katika eneo hili, kuanzia kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina hadi vita vya kichokozi vya Iraq dhidi ya Iran kati ya mwaka 1980-1988, sambamba na vita vya sasa vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen na kueleza bayana kuwa, matukio hayo yamefanyika chini uangalizi na baraka kamili ya Marekani.

Kuhusu hatua za hivi karibuni za uingiliaji wa mambo wa Washington kwa masuala ya ndani ya Lebanon zilizochukuliwa na Dorothy Shea, Balozi wa Marekani mjini Beirut, Yazbek amesema, "Marekani inajaribu kuvuna ilichoshindwa kupitia vita, silaha, sarafu ya dola na vikwazo vya kiuchumi."

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, vita vya Ghuba ya Uajemi, vita dhidi ya Lebanon vya Julai 2006, tangazo la kuzaliwa eneo la Mashariki ya Kati lililotolewa na ubalozi wa Marekani, kukaliwa kwa mabavu Afghanistan na Iraq, vita vya pande zote vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Syria, na vita dhidi ya Yemen, yote haya yamesababishwa na Washington.

3909943

captcha