IQNA

Awamu ya kwanza ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran

17:13 - July 16, 2020
Habari ID: 3472968
TEHRAN (IQNA) – Duru ya kwanza ya mashindano ya 43 ya Qur'ani Tukufu ya Tehran, mji mkuu wa Iran, imekamilika Julai 14.

Mashidano hayo ambayo yaliandaliwa na Idara ya Wakfu ya Tehran yamefanyika kwa muda wa siku tatu ambapo yalikuwa na washiriki 500.

Katika mashidano hayo ambayo yalisimamiwa na jopo la majaji 35, washiriki walishindana katika qiraa na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na pia adhana na Imamzadeh Ruhollah mjini Tehran.

Washindi watashiriki katika fainaly ya mashindano ya mkoa itakayofanyika baadaye.

Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, nchi hii iekuwa mstari wa mbele katika kustawisha utamaduni na ustaarabu wa Qurani na moja ya njia zinazotumika ni kupitia mashindano ya Qur'ani Tukufu ambayo hufanyika katika ngazi za mitaani, mijini, mikoani, kitaifa na kimataifa.

3910630

captcha