IQNA

Rais Assad wa Syria: Marekani inahitaji magaidi katika eneo

11:12 - August 14, 2020
Habari ID: 3473067
TEHRAN (IQNA) –Rais Bashar al Assasd wa Syria amesema Marekani inahitaji uwepo wa magaidi, hasa wa ISIS, katika eneo la Asia Magharibi na imetumia vikwazo vya hivi karibuni dhidi ya Syria ili kuwaunga mkono magaidi.

Rais wa Syria aliyasema hayo siku ya Jumatano katika hotuba aliyotoa kwenye kikao cha ufunguzi wa bunge la nchi hiyo. Bashar al Assad amekosoa sera za Marekani, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi yake na kuitaja sheria ya Marekani ya Caesar kuwa ni "Uharamia wa Baharini".

Rais wa Syria, Marekani ina utegemezi kwa makundi ya kigaidi katika siasa zake za nje, kiasi kwamba inaliunga mkono hata kundi la ISIS au Daesh ambalo inalitaja kama kundi la magaidi wabaya.

Rais wa Syria ameitaja sheria ya Caesar kama awamu mpya ya utoaji mashinikizo makali zaidi dhidi ya nchi yake na akasema, vikwazo hivyo havitenganiki na hatua zingine za Marekani dhidi ya Syria, na kwamba kila pale Washington inapokuwa imeshindwa kufikia malengo yake huwa inatumia silaha ya vikwazo. Assad ameufananisha utumizi wa vikwazo unaofanywa na Marekani na mbinu iliyokuwa ikitumiwa hapo zamani na maharamia wa baharini.

/3472270

captcha