IQNA

Washiriki 1,000 katika maonyesho ya Qur’ani ya Iran kwa njia ya intaneti

15:23 - April 25, 2021
Habari ID: 3473848
TEHRAN (IQNA)- Maoneysho ya kwanza ya kimatiafa ya Qur’ani Tukufu ya Iran kwa njia ya intaneti yamepangwa kuanzia Mei 1.

Hayo yamedokezwa na Abdulhadi Faqihzadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayeshighulikia masuala ya Qur’ani na Itrat amesema kutakuwa na washiriki zaidi ya 1,000 katika maonyesho hayo na miongoni mwao kuna taasisi za Qur’ani, vituo vya Qur’ani na wachapishaji.

Aidha amedokezao kuwa kutakuw ana vikao 30 vya kitaalamu kwa njia ya intaneti na kuhudhuriwa na wanazouoni na wataalamu kutoka nchi 10.

Maonyesho hayo yamepangwa kuanza tarehe 18 hadi 27 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka jana yalifutwa kutokana na janga la COVID-19 au coron lakini sasa yanafanyika kwa njia ya itaneti.

Mauzo katika maonyesho hayo ya Qur'ani yatafanyika kwa njia ya itaneti ambapo mashirika yanayouza bidhaa yanalazimika kupunguza bei kwa asilimia 20.

Maoneysho hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu nchini Iran.

Imeamuliwa kuwa hata baada ya kumalizika janga la corona, maonyesho hayo yatakuwa yakifanyika kwa njia ya intaneti na pia katika ukumbi siku za usoni.

Kutokana na janga la corona, shughuli nyingi duniani sasa zinafanyika kwa njia ya intaneti jambo ambalo limepelekea ongezeko kubwa la mauzo ya bidhaa kwa njia hiyo.

3966872

 

captcha