IQNA

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Iran itaendelea kuunga mkono kikamilifu mapambano ya taifa la Palestina

21:12 - May 22, 2021
Habari ID: 3473935
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran usiku wa kuamkia leo imetoa taarifa rasmi ya kulipongeza taifa la Palesstina hasa wakazi mashujaa na wenye subira wa Ukanda wa Ghaza kwa kusimama imara mbele ya mashambulio ya kinyama ya Israel.

Iran itaendelea kuunga mkono kikamilifu mapambano ya taifa la PalestinaKatika taarifa yake hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imesema, tunatoa pongeza kwa muqawama wa Palestina katika kulinda matukufu ya taifa hilo na kuulazimisha utawala vamizi wa Kizayuni ambao unaikalia kwa mabavu Quds, kuingia katika mlingano mpya wa mapambano ulioainishwa na wanamuqawama wa Palestina.

Vile vile Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa, Tehran itaendelea kuunga mkono kikamilifu mapambano ya taifa la Palestina, matukio ya hivi karibuni yamefufua mshikamano na umoja baina ya maeneo mbalimbali ya Palestina, kadhia ya Palestina imezuka tena na kwa upana mkubwa zaidi katika eneo hili na dunia nzima kiujumla, uungaji mkono mkubwa wa walimwengu kwa wanamuqawama wa Palestina, kufedheheka zaidi utawala wa Kizayuni na kupata nguvu upya uhakika kwamba Quds ndiyo kadhia muhimu zaidi baina ya Wapalestina na ulimwengu mzima wa Kiislamu, yote hayo ni katika matunda ya mapambano na muqawama wa Wapaletina hasa wa Ukanda wa Ghaza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kuwa, muqawama na ushindi wa wananchi wa Palestina umeonesha kwa uwazi kabisa kwamba kitendo cha kujidhalilisha baadhi ya nchi za Kiarabu zilizotangaza uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Kizayuni hakina manufaa yoyote zaidi ya fedheha. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia imesema, inataraji nchi hizo za Kiarabu zitaheshimu muqawama wa wananchi wa Palestina na malengo matukufu ya ukombozi wa Quds na zitaachana na njia na misimamo yao ghalati.

3474781/

captcha