IQNA

Jeshi katili la Israel lamuua mwandishi habari Shireen Abu Akleh

14:39 - May 11, 2022
Habari ID: 3475234
TEHRAN (IQNA)- Askari wa jeshi katili lla utawala wa Kizayuni wa Israel wamemuua kigaidi mwandishi mashuhuri na nguli wa televisheni ya al Jazeera, Shirin Abu Akleh alipokuwa katikati ya kazi zake kwenye kambi ya Jenin.

Televisheni ya al Jazeera imetangaza kuwa, pamoja na kwamba Shirin Abu Akleh alikuwa amevaa kikoti cha waandishi wa habari na cha kuzuia kupenya risasi, lakini askari wa jeshi katili la Israel wamepiga risasi kichwani kwa kutokea nyuma na kwa makusudi.

Shaatha Hanaysha, mwandishi ambaye alikuwa pamoja na Abu Akleh ameiambia televisheni ya al Jazeera kuwa, wanajeshi wa Israel walikusudia kabisa kuua. Waandishi hao walikuwa kwenye eneo la wazi, wala Wapalestina hawakuwa wanafyatua risasi. Hivyo hakukuwa na sababu kabisa kwa wanajeshi hao kufyatua risasi na tena kumlenga kichwani kabisa mwandishi huyo.

Amesema, sote tulikuwa tumevaa vikoti vya waandishi wa habari na vya kujikinga na risasi pamoja na kofia maalumu za maeneo kama hayo. Hata kwa mbali tulionekana kuwa ni waandishi wa habari. Wanajeshi wa Israel walikuweko mbele na nyuma yetu, na hakukuwa na sababu kabisa ya kutupiga risasi.

3478855

captcha