IQNA

Rais Raisi akutana na ulamaa wa Ahul Sunna Iran, asisitiza umoja na kuzuia wakufurishaji

21:57 - May 15, 2022
Habari ID: 3475255
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na maulamaa na wanazuoni wa Ahul Sunna wal Jamaa nchini Iran na kusisitiza kuwa umoja wa Shia na Sunni ni suala la kimkakati huku akitilia mkazo umuhimu wa kuzuia kujipenyeza wakufurishaji nchini.

Katika mkutano huo wa Jumapili mjini Tehran, Rais Raisi amesema wananchi wa jamii ya Ahul Sunna wa Iran wana nafasi yenye umuhimu katika historia ya nchi hii  na kuongeza kuwa maulamaa na wanazuoni wa Ahul Sunna wametoa huduma nyingi kwa muda mrefu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wamepelekea Mashia na Masunni kuishi pamoja kwa maelewano.

Akijibu ombi la maulamaa wa Ahul Sunna ambao wametaka Masunni zaidi wateuliwe katika nyadhifa za usimamizi nchini amesema: "Kutegemea ustahiki ni jambo muhimu na dharura na kigezo kianchotumiwa na serikali ni uweze wa kutenda kazi na hivyo nasisitiza kuwa kila mkoa utumie wakazi wake asili katika nyadhifa."

Katika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria kuhusu makundi ya wakufurishaji katika eneo na kusema: "Tunapaswa kuchukua  tahadhari  kuhusu kujipenyeza fikra za ukufurishaji na usalafi nchini Iran." Ameongeza kuwa, "Mashia wanaopata himaya ya serikali ya Uingereza na Masunni wanaopata himaya ya serikali ya Marekani ni pande mbili za sarafu na makundi hayo mawili yanapinga umoja katika ulimwengu wa Kiislamu."

Katika kikao hicho maulamaa na wanazuoni wa Ahul Sunna nchini Iran wamebainisha upinzani wao kwa fikra za ukufurishaji na misimamo mikali ya kidini.

4057078

captcha