IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Makka wazawadiwa

13:42 - September 26, 2022
Habari ID: 3475843
TEHRAN (IQNA) - Waandaaji wa Mashindano ya 42 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Mfalme Abdul Aziz huko Makka, Saudi Arabia wametangazwa na kutunukiwa zawadi.

Mashindano hayo yaliandaliwa katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram) kwa siku tano, na sherehe ya kufunga ilifanyika Jumapili.

Jopo la majaji limewataja al-Sayyid Muhammad al-Sanhouri kutoka Misri, Mohammed Marouf Omarev kutoka Kyrgyzstan, Ahmed Ashiri kutoka Morocco, Muhammad Khalil Habish kutoka Libya, na Ahmed Samoa kutoka Thailand kuwa washindi wakuu katika makundi matano ya shindano hilo.

Wao na washiriki wengine walioshika nafasi za juu walipokea tuzo zao, ikiwa ni pamoja na zawadi za pesa taslimu, katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Amir wa Makka.

Kwa mujibu wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, washiriki 153 kutoka nchi 111 walishiriki katika mashindano hayo. Walijumuisha wale walio na Shahada za Uzamivu na Uzamili katika fani za Qur'ani.

Wizara hiyo imeandaa Mashindano ya Kimataifa ya Mfalme Abdul Aziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kufasiri Qur'ani Tukufu kila mwaka tangu mwaka 1399 Hijria (1979).

 4087999

captcha