IQNA

Usomaji Qur'ani (Qiraa)

Usomaji wa Qur'ani wa Sheikh Mustafa Ismail zaidi ya nusu karne iliyopita (+Video)

TEHRAN (IQNA) - Kanda za video zimesambazwa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha usomaji wa aya za Qur'ani Tukufu wa marehemu Sheikh Mustafa Ismail aliyekuwa qarii bingwa wa Qur'ani Tukufu wa Misri

Katika klipu hiyo ya 1971, qarii huyo maarufu anasema Sura za Ad-Dhuha na Al-Inshirah katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wakuu wa Misri.

Sheikh Mustafa Ismail alikuwa qari ambaye alianzisha mtindo bunifu wa usomaji ambao kwa namna fulani angeonyesha dhana au madhumuni ya aya kupitia sauti yake nzuri.

Sheikh Mustafa Ismail aliyezaliwa Juni 17,1905 katika eneola Tanta jimboni Gharibia nchini Misri na alikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri zaidi wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Alikuwa na mtindo maalumu wa qiraa na aliweza kuwavutia wengi kutokana na usomaji wake. Qarii mashuhuri wa Misri katika zama hizi Sheikh Ahmed Ahmed Noaina amesema, "Mustafa Ismail alikuwa na mbinu kadhaa za qiraa na hadi sasa hakuna mtu aliyweza kuja na mbinu mpya baada yake.

Alianza kujifunza Qur'ani Tukufu na misingi ya Tajwidi kutoka kwa Sheikh Idris Fakhir. Alizana qiraa ya Qur'ani mbele ya hadhara kubwa akiwa na umri wa miaka 4 katika Msikiti wa Atif eneo la Tanta ambapo sauti yake iliwavutia wengi. Aliendeleza kipaji chake kwa kuelekea Cairo ambapo alikuwa mwanafunzi wa Qarii Sheikh Muhammad Rafa'at. Alipata umashuhuri na akaanza kualikwa katika nchi mbali mbali kusoma Qur'ani Tukufu kama vile Iraq, Indonesia, Saudi Arabia, Pakistan, Ujerumani, Palestina, Uingereza na Ufaransa.  Aidha alitunukiwa tunzo kadhaa kitaifa na kimataifa kutokana na umahiri wa qiraa yake ya Qur'ani Tukufu. Hatimaye Sheikh Mustafa Ismail aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake mnamo Disemba 26, 1978.

 4097407