Aidha saini ya mchoraji wa nyumba hii inaonekana na maneno "Raqmeh Zainul Abdin 1268".
Eneo la nyumba hii lilikuwa zaidi ya mita za mraba 2000 hapo awali, lakini leo ni mita za mraba 530 tu. Familia ya Ejei ni moja ya familia mashuhuri za mjini Isfahan waliokuja Isfahan kutoka eneo la Eje mkoani Isfahan. Familia ya Ejei ni mashuhuri kama wanazuoni wa kidini, na baadhi yao walikuwa maimamu wa msikiti wa "Ali" katika kitongoji cha "Harunieh.