IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 36

Ni marufuku katika Qur'ani kwa Waislamu kufunga ndoa na washirikiana

15:59 - November 19, 2022
Habari ID: 3476112
TEHRAN (IQNA) – Familia ni mojawapo ya misingi muhimu ya jamii na inabeba jukumu la kulea watoto wanaojenga vizazi vijavyo. Uislamu unalipatia umuhimu mkubwa kitengo hiki cha kijamii na umefafanua mifumo maalum kwa ajili yake.

Qur'ani Tukufu inatoa kanuni nyingi juu za ndoa; mmoja wao ni kuwakataza Waislamu kuoa wale wanaomshirikiza Mwenyezi Mungu.

"Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.” (Surah Baqarah, aya ya 221)

Akifafanua juu ya aya hiyo, katika Tafsir Nemooneh, Ayatullah Makarem Shirazi anabainisha kwamba sehemu hii ya Surah Baqarah ni jibu la swali la kuoa mushrikina. Ayah ii inamaanisha kwamba ndoa hailengi tu kukidhi mahitaji ya mtu ya ngono kwani mwenzi ana jukumu la moja kwa moja katika kukuza watoto na kuunda tabia ya mtu.

Kinachokuja mwishoni mwa Aya ni amri ya kufikiri kwa undani zaidi: “Washirikina wanakuiteni Motoni, lakini Mwenyezi Mungu anakuiteni kwenye Pepo na msamaha kwa mapenzi yake.

Wakati huo huo, Tafsir Noor  ya Hujjatul Islam Mohsen Qara’ati inaorodhesha jumbe 13 za aya hii:

  1. Waislamu hawana haki ya kuwa na mahusiano ya kifamilia na wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu.
  2. Imani ni muhimu zaidi katika kuchagua mchumba, na ndoa na ni haramu kufunga ndoa na mushrikina.
  3. Mtu asidanganywe na uzuri, mali, na nafasi ya upande mwingine
  4. Uzuri, mali, na cheo haviwezi kuchukua nafasi ya imani
  5. Mtu anapaswa kuwa makini na wasiojiweza kwani ndoa na waumini inapendekezwa
  6. Tamaa za kibinadamu zinapaswa kudhibitiwa ndani ya mfumo wa imani
  7. Imani ndiyo inayoleta thamani na ukafiri ndio ufunguo wa kuanguka
  8. Kwanza waamini ndipo ndoa inaweza kutokea. Mtu asifikirie kuwa imani inaweza kuja baada ya ndoa
  9. Waislamu wazuie kupenya kwa ibada yenye shirki katika maisha yao na wazingatie hatari za ndoa hizo.
  10. Ndoa na wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu hutayarisha mazingira ya kuelekea jahanam.
  11. Kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu ndiyo njia ya kwenda Peponi
  12. Msamaha hutolewa tu na Mwenyezi Mungu, tofauti na Ukristo ambao viongozi wa imani wanaaminika kuwa na nguvu kama hiyo.
  13. Wanadamu kwa asili yao ya kimaumbile wanaelewa mambo na kanuni huja kama ukumbusho tu
Habari zinazohusiana
captcha