IQNA

Qur'ani nchini Misri

Mwalimu Bora wa Qur'ani mwaka 2022 nchini Misri

19:07 - November 23, 2022
Habari ID: 3476135
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Wakfu wa Misri alimteua Mustafa Muhammad Mustafa Abdullah Abu al-Amayim kama mwalimu wa mfano wa Qur'ani wa nchi hiyo mnamo 2022.

Al-Amayim pia ni kiongozi wa maombi na mhubiri wa idara ya Awqaf katika Jimbo la Kafr el-Sheikh nchini, tovuti ya Al-Qahira iliripoti.

Waziri wa Awqaf Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa alisema al-Amayim ndiye mshindi bora wa shindano lililofanyika kote nchini la kuchagua mwalimu bora wa Qur'ani katika mwaka huu.

Alishinda tuzo ya juu, ambayo ni tuzo ya pesa taslimu yenye thamani ya pauni 100,000 za Misri, Sheikh Gomaa alibainisha.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Wakfu kuwaenzi walimu wa Qur'ani na kuthamini huduma zao kwa Qur'ani.

Al-Amayim, ambaye anatoka kijiji cha Ibshan huko Kafr el-Sheikh, kaskazini mwa Misri, ni mhitimu wa Kitivo cha Usul al-Din na Uenezi wa Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar.

Alipata Shahada ya Uzamili ya Ufafanuzi na Sayansi ya Qur'ani mwaka wa 2003 na akaendelea kupata Uzamivu (PhD) yake katika fani hiyo hiyo mwaka wa 2006.

Alishinda tuzo hiyo kwa miaka 32 ya juhudi katika kutumikia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuhifadhi Qur'ani.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Kurani ni za kawaida sana katika nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi.

4101564

captcha