Hafla hiyo ilifanyika Ijumaa jioni kuzindua Msikiti wa Bahri huko Tant Al-Jazira katika mkoa wa kaskazini, tovuti ya habari ya al-Bawaba iliripoti.
Qalyubia iko kaskazini mwa Cairo katika eneo la Delta ya Nile na mji mkuu wake ni Banha.
Mahmoud Shahat Anwar, Yassir al-Sharqawi, Shahat al-Sayyed A’azazi na Sheikh Mohamed Abdul Qadir walikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
Kulikuwa pia na wanaharakjati wengine wa Qur'ani, wanazuoni na wasomi wa Qur'an na shakhsia wengine kidini katika televisheni waliohudhuria sherehe hiyo.
Maqarii walisoma aya za Qur'ani Tukufu na Sheikh Mohamed Abdul Qadir aliwasilisha Ibtihal katika sherehe ya uzinduzi.
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.
Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi hii ambayo ina idadi kubwa zaidi ya wasomaji bingwa wa Qur'ani Tukufu duniani.
4102353