IQNA

Kongamano la Qur'ani

Mamia wahudhuria kongamano la namna Qur’ani Tukufu inavyoweza kutatua changamoto za kisasa

20:40 - December 05, 2022
Habari ID: 3476198
TEHRAN (IQNA) – Tukio lililopewa jina la “Kongamano la Kimataifa la Qu’ani” lilifanyika Kuala Lumpur siku ya Jumamosi kwa kushirikisha mamia ya watu.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF) ilijadili masuluhisho ya Qur'ani kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kisasa kwa kuzingatia ujumbe wa Surah As-Sajdah.

Marhaini Yusoff, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, alisema tukio hilo la kimataifa lililenga kutoa masuluhisho ya Kiislamu na Qur'ani kwa changamoto za kifedha, kikazi, kifamilia, kijamii na kiroho.

Hili lilikuwa tukio la mwisho mwaka huu chini ya mfumo wa kampeni ya "#QuranHour", alisema.

Akizungumzia changamoto mbalimbali za kiuchumi na majanga ya kimaumbie ambayo watu wanaweza kukabiliana nayo katika miaka ijayo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa msaada wa Mwenyezi  Mungu unahitajika kutatua baadhi ya matatizo hayo.

Matukio kama haya yanatarajiwa kusaidia jamii kupata suluhisho kama hilo la kiroho, aliongeza.

Akiashiria programu za WUIF ambazo zinalenga kukuza usomaji, uelewa na utekelezaji wa Qu’ani  Tukufu, Yusoff alitumai kuwa taasisi hiyo inaweza kuandaa hafla kama hizo katika nchi zingine.

Alisema Iran, India, Singapore, na Brunei ni miongoni mwa nchi ambazo zimeonyesha nia yao ya kuandaa mikutano kama hiyo.

Yusoff pia alisema kutokana na kukaribishwa kwa vita vya watu kwa tukio la siku moja la mwaka huu, toleo la mwaka ujao litafanyika Desemba 2-3, 2023.

Wataalamu kutoka Malaysia, Indonesia, Bangladesh, Misri, Marekani, na Palestina walihutubia kongamano la mwaka huu.

4104323

captcha