IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 45

Taswira ya wazi ya Siku ya Kiyama katika Sura Al-Jathiyah

17:15 - December 06, 2022
Habari ID: 3476208
TEHRAN (IQNA) - Vitabu vya kidini na vya Mwenyezi Mungu vimezungumzia maisha ya akhera lakini wengine wanakanusha na kusema hizi ni hadithi na ngano za kale.

Hata hivyo, Qur'ani Tukufu imetoa picha au taswira ya wazi ya ulimwengu huo katika Sura tofauti, ikiwa ni pamoja na Surah Al-Jathiyah.

Jina la sura ya 45 ya Quran ni Al-Jathiyah. Ina Aya 37, ni Makki na iko katika 25 Juz. Ni Sura ya 65 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Jathiyah katika aya ya 28. Ina maana ya kupiga magoti na aya hii inaeleza jinsi watu watakavyopiga magoti ili kupokea kitabu chao (ambacho yameandikwa ndani yake waliyoyafanya wakiwa duniani).

Makusudio ya Sura hii ni kuwalingania watu wote katika dini ya Tauhidi na waepuke adhabu.  Sura Al-Jathiyah imeanza na suala la Tauhidi na kisha inabainisha suala la utume na haja ya kuwafuata Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Vile vile inawaonya na kuwatishia wale wanaozikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kufuata matamanio ya nafsi zao  ingawa wanatambua kuwa wanafuata njia potofu.

Sura inasawiri kipengele cha jinsi makafiri wanavyokabiliana na wito wa kufuata Uislamu na ukaidi wao katika kuukabili ukweli na kufuata matamanio yao ya kidunia.

Surah Al-Jathiyah inawasilisha mwaliko kutoka kwa Mwenyezi  Mungu kwa wanadamu. Inatoa sababu na mantiki pamoja na kutia moyo na maonyo ili kuwaongoza watu kwenye ukweli.

Inarejelea kundi la watenda dhambi ambao kwa kiburi wanapuuza au kukana ishara za Mwenyezi Mungu Inasisitiza kwamba wataadhibiwa vikali Siku ya Kiyama.

Sura inafungua njia ya uongofu na inataja baadhi ya ishara za Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, inawaita watu kutafakari. Vile vile inaashiria Siku ya Kiyama na inawaonya wanao kadhibisha.

Katika Surah Al-Jathiyah Siku ya Hukumu imechorwa kwa uwazi. Tunaona makundi yote ya watu wanaosubiri kutathminiwa matendo yao. Wanapokea “kitabu” chao ambamo matendo yao yote katika ulimwengu huu yameandikwa.

Kisha Sura inawagawanya watu makundi mawili: Waumini wanaopata malipo na rehema ya Mwenyezi Mungu na makafiri wanaokabiliwa na adhabu na makazi yao ni Jahannamu.

Habari zinazohusiana
captcha