IQNA

Hiija na Umrah

Takriban Mahujaji Milioni 30 wanufaika na huduma za kujitolea katika Masjid Al-Haram

22:41 - December 07, 2022
Habari ID: 3476212
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde zaidi zilizotolewa na mamlaka ya Saudia, Waislau watu milioni 30 wanaoshiriki ibada ya Hija ndogo ya Umrah wamepokea huduma za hiari katika Msikiti Mtakatifu Mkuu wa Makka, Al Masjid al Haram, mwaka huu wa Hijria Qamaria.

Idara ya Kijamii, Kujitolea na Kibinadamu, inayohusishwa na Urais wa Misikiti Miwili Mitakatifu, imetangaza leo kwamba karibu waumini milioni 30 wamefaidika na huduma za kujitolea katika Msikiti Mtakatifu Mkuu tangu kuanzishwa mwaka jana hadi robo ya kwanza ya mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria.

Kwa mfano, kulingana na takwimu za hivi punde, milo ya kufugua saumu  au futari imetolewa kwa waumini 5,915,193. Aidha chupa 2,357,190 za maji yenye baraka ya  Zamzam zimekabidhiwa waumini katika eneo hilo  takatifu.

Jumla ya muda wa kujitolea umefikia saa 1,213,540 zilizoongezwa na mamlaka 35 za kujitolea, zinazoshughulikia nyanja 17, na kunufaisha jumla ya waumini 29,597,552, kulingana na takwimu.

3481571

Kishikizo: makka umrah hija ndogo
captcha