IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Israel wavamia Msikiti wa al-Aqsa na kucheza ngoma za uchochezi

16:54 - January 20, 2023
Habari ID: 3476433
TEHRAN (IQNA)- Makumi ya walowezi Waisraeli wamevamia eneo la Msikiti wa al-Aqsa huko Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel, katika hatua nyingine ya uchochezi dhidi ya waumini Waislamu wa Kipalestina.

Walioshuhudia wanasema kwamba uvamizi wa walowezi hao  wenye itikadi kali ulifanyika chini ya ulinzi mkali kutoka kwa wanajeshi wa utawala ghasibu wa  Israel. Walowezi hao  waliinua bendera za utawala haramu wa Israel na kucheza ngoma za uchochezi ndani ya eneo hilo.

Vikosi vya utawala vamizi wa Israel pia viliweka askari ndani na nje ya msikiti ili kulinda uvamizi wa walowezi hao.

Wanajeshi wa Israel pia waliwashambulia maelfu ya Wapalestina, wakiwemo vijana, katika eneo la la Bab al-Amoud la Msikiti wa Al Aqsa. Walijaribu kuwalazimisha Wapalestina kuondoka eneo hilo ili kuwaruhusu Wazayuni wakoloni kulitembelea. Uchochezi huo uliibua ghasia kufuatia malalamiko makalai ya Wapalestina.

Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ilitoa wito kwa Wapalestina kutoka matabaka yote ya maisha kukusanyika kwa wingi, kuongeza uwepo wao katika eneo la msikiti huo, na kulinda eneo takatifu dhidi ya uvamizi wa mara kwa mara wa walowezi wa Israel.

"Tunawapongeza watu wa Palestina katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na katika Ukingo wa Magharibi ambao wanasimama kidete kupinga ukiukaji wa uvamizi wa Israel na uhalifu," ilisema taarifa yake.

Hamas pia iliutaka Umma wa Kiarabu na Kiislamu, pamoja na watu huru wa dunia, "kuunga mkono uthabiti wa watu wa Palestina na kufanya kazi katika kuwalinda dhidi ya ukiukaji wa uvamizi wa Israel."

Siku ya Ijumaa asubuhi, maelfu ya waumini wa Kipalestina walifika katika Msikiti wa al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa katika viwanja vyake huku kukiwa na hatua kali za utawala vamizi wa Israel. Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya ndani, idadi ya Wapalestina waliohudhuria sala hiyo ilifikia 75,000.

Uvamizi wa walowezi wa Israel katika Msikiti wa al-Aqsa umeongezeka katika wiki za hivi karibuni kutokana na kuwasili kwa utawala mpya wa siasa kali za mrengo wa kulia unaoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Uchochezi huo wa walowezi wa Kizayuni kwa uungaji mkono w utawala ghasibu wa Israel huko al-Quds, na kusababisha makabiliano ya kila siku na Wapalestina katika msikiti huo, huku wengi wakijeruhiwa, kukamatwa na kuuawa.

Suala hilo limekuwa chanzo cha mvutano mkubwa kati ya utawala wa Israel na Wapalestina kwa miongo kadhaa. Aidha uchochezi huo wa walowezi wa Kizayuni ulikuwa sababu ya kuanza Intifadha au mwamko wa Wapalestina katika miaka ya 2000-2005.

/3482139

Habari zinazohusiana
captcha