IQNA

Harakati za Qur'ani

Shirika la hisani lasambaza Misahafu 11,000 barani Afrika

18:18 - January 23, 2023
Habari ID: 3476451
TEHRAN (IQNA) - Taasisi ya kutoa misaada ya Uturuki ilitoa zaidi ya nakala 11,000 za Misahafu (Qur'ani Tukufu) kwa Waislamu katika nchi tofauti za Kiafrika mwaka jana.

Wakfu wa Misaada ya Kibinadamu au IHH imesambaza Misahafi hiyo katika nchi za Nigeria, Mali, Burkina Faso, Chad, Guinea, Ethiopia, Benin na Sudan.

Taasisi hiyo ilisema katika taarifa yake kwamba, kwa nakala hizo, jumla ya nakala za Qur'ani ambazo imetoa zawadi kwa watu katika nchi mbalimbali hadi sasa zimefikia 274,000.

Imeongeza kuwa unajivunia kutimiza sehemu ya haja ya Waislamu katika baadhi ya nchi kupata Kitabu hicho Kitakatifu.

Kwa mujibu wa tovuti yake, IHH imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 1992 kwa madhumuni ya kufikisha misaada kwa watu wote wanaohitaji, waliopata maafa, wahanga wa vita, majanga ya asili n.k au waliojeruhiwa, vilema, njaa, wasio na makazi na wanaoteswa popote walipo, bila kujali dini zao, lugha, rangi au madhehebu yao, na kuzuia uvunjwaji wa haki msingi za binadamu na uhuru wa watu hao.

Shughuli za kujitolea za IHH zilibadilika na kuwa shirika rasmi mnamo 1995 na kuenea karibu na mabara matano ilipoanzisha daraja la nia njema linaloanzia Uturuki hadi nchi 123.

4116531

captcha