IQNA

Taazia

Mwanazuoni wa Qur’ani Mauritania Mohamed Mokhtar Ould Abah afariki dunia

20:52 - January 24, 2023
Habari ID: 3476454
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu Mauritania ambaye amenadika tarjuma ya Qur’ani Tukufu Mohamed Mokhtar Ould Abah amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.

Msomi huyo, ambaye ametarjumu Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa, aliaga dunia Januari 22.

Alizaliwa mwaka wa 1924 katika jimbo la Boutilimit la Mauritania na alihifadhi Qur’ani Tukufu akiwa kijana kisha akajifunza sayansi za Kiislamu.

Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Muhammad V huko Morocco katika fani ya fasihi ya Kiarabu na ustaarabu na kisha akapata Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Sorbonne nchini Ufaransa, ambapo aliandika tasnifu yake kuhusu historia ya masomo ya Sharia ya Kiislamu nchini mwake.

Mohamed el Mokhtar Ould Abah alichangia katika kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kwanza cha elimu ya Kiislamu nchini Mauritania na kuchukuliwa kuwa mwanzilishi katika taaluma ya lugha ya Kiarabu na masomo ya utamaduni wa Kiislamu nchini humo.

Aliandika vitabu 50 hivi katika nyanja kama vile sayansi ya Qur’ani Tukufu, Hadith, Seerah, Fiqh, misingi kidini, lugha na fasihi.

Tarjuma yake ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa inachukuliwa kuwa miongoni mwa bora zaidi.

Moja ya vitabu vyake, “Vitabu vya Kisheria na Mabadiliko  katika Madhehebu ya Maliki Mauritania “, kilichochapishwa mwaka wa 1981, ni marejeleo makuu kwa watafiti wanaopenda mikondo ya kidini.

Pia alikuwa mwanasiasa aliyeheshimika sana, akihudumu mara kadhaa kama naibu na waziri nchini Mauritania. Mwanzoni mwa miaka ya sitini, Mfalme Hassan II alimteua kuwa mkurugenzi wa redio ya kitaifa.

 4116717

captcha