IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /21

Qiraa ya Qur’ani ya Ustadh Abdel Aziz Akasha kwa msingi wa maana

21:55 - January 24, 2023
Habari ID: 3476457
TEHRAN (IQNA) – Abdel Aziz Akasha alikuwa qari wa Misri ambaye alipata umaarufu baada ya kuanzisha mtindo maalum katika usomaji wa Qur’ani Tukufu.

Usomaji wake ulikuwa unaenda sambamba na maana, yaani, angebadili sauti yake kulingana na maana ya Aya.

Alikuwa miongoni mwa ‘kizazi cha dhahabu’ cha wasomaji Qur’ani wa Misri pamoja na mabwana kama vile Abolainain Shoaisha, Shahat Muhammad Anwar, na Muhammad Al-Hilbawi.

Akasha alizaliwa mwaka wa 1948. Alienda Maktab (shule ya jadi ya Qur'ani) akiwa na umri wa miaka minne ili kuhifadhi Qur’ani Tukufu na baada ya kujifunza Tajweed, alipokea cheti cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu akiwa na miaka 9.

Akiwa na umri wa miaka 16, alikwenda Cairo na kuanza kuadhini kwenye msikiti katika mji mkuu wa Misri.

Baadaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar.

Ustadh Akasha alikuwa na sauti ya kuvutia na yenye nguvu. Miongoni mwa sifa bainifu za usomaji wake ni kwamba alibadili sauti alipokuwa akisoma Qur’ani na halikadhalika alitilia mkazo maana wakati wa usomaji wake.

Ustadh Akasha alitembelea Iran mara tatu katika maisha yake. Ziara yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2011 ambapo alisoma aya za Qur'ani Tukufu mbele ya Kiongozi Muadhamu  wa Mapinduzi ya Kiislamu.

UstadhAkasha alirejea kwa Mola wake  mnamo 2013 akiwa na umri wa miaka 63.

Hapa chini ni  usomaji wake wa aya katika Sura Al-Buruuj na Sura At-Takathur:

captcha