IQNA

Uislamu Marekani

'Mgeni Katika Lango': Filamu ya Msikiti wa Muncie, Marekani yateuliwa Tuzo ya Oscar

21:57 - January 26, 2023
Habari ID: 3476469
TEHRAN (IQNA) – Filamu fupi kuhusu kisa cha kweli cha mwanajeshi wa Marekani ambaye alipanga kulipua kwa bomu Kituo cha Kiislamu cha Muncienchini Marekani lakini akapata marafiki ndani na kusilimu imeteuliwa kuwania Tuzo ya Academy nchini Marekani.

Filamu hiyo aina ya dokumentari imeongozwa na kutayarishwa na Joshua Seftel, ni ya dakika 30 na imepewa jina la "Stranger at the Gate" ambapo inasimulia kisa cha kweli cha askari veteran wa Marekani Richard "Mac" McKinney ambaye alitaka kulipua msikiti.

Badala ya kupata maadui msikitini, McKinney alikutana na wanachama kadhaa wa Kituo cha Kiislamu cha Muncie ambao walimkaribisha ndani.

Akiwa anaugua ugonjwa wa Mfadhaiko wa Baada ya Tukio la Kiwewe(PTSD) , McKinney anakutana na Bibi na Saber Bahrami, waanzilishi wenza wa Kituo cha Kiislamu cha Muncie, na Jomo Williams, Mmarekan-Mwafrika  aliyesilimu.

"Wakati Josh Seftel, mkurugenzi wa 'Stranger at the Gate,' alipowasiliana nami kama rais wa Kituo cha Kiislamu cha Muncie na wazo la filamu hii fupi, nilikumbatia fursa ya kuonyesha jinsi jumuiya yetu ya Kiislamu huko Muncie iliweza kumkaribisha  Mac kwa  mikono wazi,” Bibi Bahrami aliambia The Star Press.

Bibi Bahrami alisherehekea uteuzi Jumanne na kusema ni  fursa ya kuendelea kuishi kwa amani na maelewano.

"Mimi na mume wangu tumebarikiwa kabisa kuweza kuchangia na kuleta mabadiliko katika kuboresha uelewa na kupunguza chuki katika jamii nchini Marekani," Bibi Bahrami, mwanzilishi na rais wa AWAKEN Inc., alisema.

"Baada ya 9/11, jumuiya yetu ya Kiislamu ilikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama na maisha ya watoto wetu na wajukuu, na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu na kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu."

Aliongeza kuwa filamu hiyo inaonyesha wema wa watu, ikiunga mkono ujumbe wa uelewa.

"Ninahisi unyenyekevu na kubarikiwa kwamba mume wangu Saber, mwanangu Zaki, na mimi ni sehemu ya ujumbe huu wa ajabu unaoonyesha jinsi upendo na uelewano unavyoweza kushinda chuki kila wakati," alisema.

"Stranger at the Gate" ni ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa filamu fupi za za visa vya kweli ambazo zimetayarishwa na Seftel zinazojulikana kama "Siri ya Maisha ya Waislamu."

Filamu hizo fupi zaomaamgazia Waislamu mashuhuri , akiwemo AJ+ Dena Takruri, mshindi wa medali ya olimpiki Marekani Ibtihaj Muhammad, na mwandishi Reza Aslan.

/3482224

captcha