IQNA

Iran ya Kiislamu

Wananchi waandamana kote Iran kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

16:49 - January 27, 2023
Habari ID: 3476471
TEHRAN (IQNA)- Baada ya kuswali Sala ya Ijumaa, wananchi kote katikaa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamejitokeza mitaani na kulaani hatua za hivi karibuni za nchi za Magharibi na Ulaya zikiongozwa na Marekani za kudhalilisha matukufu ya Kiislamu na kuliwekea vikwazo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Waumini waliojitekeza kwa wingi baada ya Sala ya Ijumaa wamelaani vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya.
Huku wakiwa wamebeba mabango  na wakiwa wantamka Takbir, waandamanaji walisema wako tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya Qur'ani Tukufu, Uislamu, Mtume SAW pamoja Ahul Bayt AS na Kiongozi Muadhamu.  Waandamanaji aidha walitoa nara za 'Mauti kwa Marekani' na 'Mauti kwa Israel', huku wakilaani vikali vitendo vya kujunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Jumamosi iliyopita Rasmus Paludan, mwanasiasa mwenye misimamo mikali wa Denmark alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu karibu na Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm huku akiwa analindwa na polisi ya Uswidi. 

Aidha siku ya Jumapili, Edwin Wagensveld, mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Uholanzi, na kiongozi wa kundi la chuki dhidi ya Uislamu la Pegida, alirarua kurasa za Qur’ani Tukufu huko The Hague, mji mkuu wa Uholanzi. Video ya Wagensveld kwenye Twitter ilionyesha kuwa alichoma kurasa zilizochanwa za Qur’ani Tukufu.

Vitendo hivi vinaendelea kulaaniwa vikali na Waislamu pamoja na nchi za Kiislamu duniani ambapo serikali za Sweden na Uholanzi zimekosolewa kwa kuunga mkono vitendo hivyo viovu.

Wakati huo huo, wananchi wa Iran ya Kiislamu pia wamelaani hatua ya Bunge la Ulaya kuliweka jina la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika orodha ya kile inachodai ni "mashirika ya kigaidi". Tayari Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa hatua ya kihisia ya taasisi hiyo ya kupiga kura ya kuliongeza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika orodha ya eti mashirika ya 'kigaidi' ya Umoja wa Ulaya itakuwa na matokeo mabaya, na kwamba Ulaya italipa gharama kubwa kwa hatua zake hizo.

4117547

captcha