IQNA – Toleo la 15 la Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya “Safir” limehitimishwa rasmi katika Msikiti Mkuu wa Kufa nchini Iraq.
Habari ID: 3482734 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/09/07
Katika mazingira ya kiroho yaliyojaa baraka, Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, Iraq, imeandaa hafla ya kila wiki ya Qur’an inayojulikana kama “Arsh ya Qira’a” (Mbingu ya Usomaji).
Habari ID: 3482733 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/09/07
IQNA-Taasisi ya Al-Warith ya uchapishaji wa Qur’anI Tukufu, inayofanya kazi chini ya Haramu Takatifu ya Imam Hussain (AS) nchini Iraq, imetangaza kuwa imepata mafanikio makubwa katika mpango wake wa kuchapisha nakala za Qur’ani Tukufu ndani ya nchi , hatua inayowakilisha mabadiliko makubwa ya kiviwanda na ya kidini kwa taifa hilo.
Habari ID: 3482731 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/09/07
IQNA – Banda la Idara ya Ataba (Haram) Tukufu ya Imam Ali (AS) limeweka wazi nakala ya muswada wa Qur’an Tukufu inayohusishwa na Imamu huyo katika Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Vitabu ya Baghdad.
Habari ID: 3482727 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/09/06
IQNA – Kikao maalumu cha kufanya tathmini ya mbinu za kielimu katika vituo vya Qur’ani vinavyosimamiwa na Astan (Idara ya Mfawidhi) wa Haram ya Imam Hussein (AS) kimefanyika katika mji wa Karbala.
Habari ID: 3482681 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/26
IQNA – Kozi maalum ya maandalizi ya waamuzi wa mashindano ya Qur’ani nchini Iraq imefikia tamati kwa hafla adhimu.
Habari ID: 3482647 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/19
IQNA – Msichana mmoja wa shule ya upili nchini Iraq amefikia hatua ya kipekee na ya kusifiwa kwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima katika kipindi cha siku 43 pekee. Zainab, mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Khadija nchini Iraq, alipewa heshima kubwa kwa mafanikio yake haya adhimu.
Habari ID: 3482594 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07
IQNA-Mashindano makubwa ya kuhifadhi Quran Tukufu yameanza rasmi siku ya Jumamosi katika mkoa wa Nineveh nchini Iraq, yakishirikisha jumla ya mahafidhi elfu ishirini kutoka rika zote
Habari ID: 3482579 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/03
IQNA – Balozi wa Iran nchini Iraq amesema kuwa Mashaya au matembezi ya Arbaeen ya mwaka huu yanaendeshwa kwa utukufu mkubwa zaidi, kwa utaratibu mzuri na ikiwa na changamoto chache ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Habari ID: 3482575 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/02
IQNA – Mkutano wa wanazuoni wa Kisunni na Kishia kutoka Iran na Iraq ulifanyika siku ya Ijumaa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Habari ID: 3482545 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/27
IQNA – Makao Makuu ya Kituo cha Arbaeen nchini Iran yametangaza kuanza rasmi kwa utumaji wa mazuwari kuelekea Iraq kwa ajili ya msafara wa Arbaeen wa mwaka huu.
Habari ID: 3482538 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/26
IQNA – Zaidi ya Mawakib (vituo vya kutoa huduma bila malipo) 13,500 kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq, pamoja na kutoka mataifa ya Kiarabu, Kiislamu na nchi nyingine za kigeni, zimesajiliwa kushiriki katika maonyesho na matembezi ya Arbaeen ya mwaka huu.
Habari ID: 3482534 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/25
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, amesema kuwa misafara ya mazishi ya Kiongozi Shahidi, iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu, imedhihirisha kikamilifu upana wa huruma, udugu, na mshikamano uliopo kati ya mataifa mawili ya Iraq na Iran.
Habari ID: 3482505 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19
IQNA – Vikosi vya Hashd al-Shaabi (Jeshi la Kujitolea la Wananchi) vya Iraq vimetangaza siku ya Ijumaa kuwa vimeanza kutekeleza mpango maalum wa kuhudumia mamilioni ya mazuwaru wanaoelekea kwenye matembezi ya Arbaeen.
Habari ID: 3482501 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/18
IQNA – Uwepo wa mamilioni ya waumini katika misafara ya mazishi iliyofanyika nchini Iran na Iraq kwa ajili ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, unabeba ujumbe muhimu, wa kina na wenye nguvu.
Habari ID: 3482483 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14
Shughuli ya kuusindikiza mwili mtukufu wa Imamu Mujahid Shahidi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (qaddasallahu nafsahu al-zakiyyah) ilifanyika siku ya Jumatano, tarehe 8 Julai , katika mji mtukufu wa Najaf al-Ashraf, kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi waombolezaji wa Iraq. Baada ya msafara wa mazishi, Ayatullah Sayyid Muhammad-Taqi al-Hakim, mmoja wa wanazuoni wa Iraq, aliswalisha Swala ya Maiti ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ndani ya haram tukufu ya Amir al-Mu’minin Ali (AS).
Habari ID: 3482467 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/10
IQNA- Mamlaka katika Jimbo la Najaf nchini Iraq zimekamilisha maandalizi ya usalama, vifaa, na huduma kwa ajili ya msafara wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei.
Habari ID: 3482448 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06
IQNA – Kufuatia kuanza kwa uratibu mpana kati ya taasisi za Iraq na Iran, Iraq inajitayarisha kuandaa misafara ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Seyed Ali Khamenei katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.
Habari ID: 3482419 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/29
IQNA – Mamilioni ya waombolezaji mjini Karbala wameshiriki adhuhuri ya Ijumaa ya Ashura katika msafara mkubwa na wa kihistoria wa Rakdhat Tuwairij.
Habari ID: 3482410 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/27
IQNA – Baba na mwanae kutoka Misri waliokuwa washiriki katika Tuzo ya Qur’ani ya Al Ameed nchini Iraq wamekuwa miongoni mwa waliopata nafasi za juu katika shindano hilo la kimataifa la usomaji wa Qur’ani.
Habari ID: 3482368 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/16