Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Imam Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru washindi walioliletea taifa medali katika mashindano ya Paralympic yaliyomalizika jana mjini London, Uingereza.
2012 Sep 10 , 16:31
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu katika mkutano wa taifa wa swala:
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe kwenye mkutano wa 21 wa taifa wa swala akisisitiza kuwa kuweka ibada hiyo katika nafasi yake inayostahiki kutatayarisha uwanja mzuri wa jamii kufikia kwenye kiwango kinachotakikana cha thamani za Uislamu.
2012 Sep 05 , 21:23
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Alkhamisi) amekutana na Rais wa Tajikistan na kusema kuwa lugha, utamaduni wenye historia ndefu na wa pamoja wa mataifa ya eneo hili ni uwanja mzuri wa kupanua na kuimarisha uhusiano wa pande mbili na pande kadhaa na kujenga mustakbali bora.
2012 Aug 31 , 15:35
Vipindi vinavyoendeshwa katika Haram za Imam Hussein, Hadhrat Abul Fadhl katika mji mtakatifu wa Karbala na Haram ya Imam Ali (as) mjini Najaf vimekuwa vikirushwa hewani moja kwa moja kupitia kanali tofauti za Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hasa Kanali ya Qur'ani.
2012 Aug 16 , 12:44
Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa misikini imeongezeka kwa taqriban asilimia 36 katika Ufalme wa Dubai katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
2012 Aug 16 , 12:36
Sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hassan bin Ali bin Abi Twalib (as) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei jioni ya leo amehutubia hadhara ya walimu wa lugha na fasihi na Kifarsi na washairi vijana waliokwenda kuonana nae.
2012 Aug 05 , 15:26
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaonyesha athari na kazi za wasanii wa Kiirani katika nyanja za Qur'ani kwenye mji wa Erzurum huko mashariki mwa Uturuki.
2012 Aug 01 , 20:03
Duru ya pili ya mashindano ya kimataifa ya picha zenye maudhui ya "umaanawi wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika nchi mbalimbali" yatafanyika Dubai kwa hisani ya Studio Basel.
2012 Jul 18 , 15:56
Maktaba ya umma ya Fatma az-Zahra (as) inayofungamana na msikiti mkuu wa Imam wa Zama, yaani Imam Mahdi (af) imefunguliwa katika mtaa wa Pule Khushk katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
2012 Jul 18 , 15:35
Vifurushi maalumu vya kiutamaduni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambavyo vimeteyarishwa na Idara Kuu ya Kiutamaduni ya Wairani Wanaoishi Nje ya Nchi vimepangwa kutolewa kwa Waislamu wa Hispania na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
2012 Jul 17 , 12:56
Sherehe maalumu za kutimu umri wa taklifu kwa vijana wa Kiislamu zilifanyika jana Jumapili katika Husseiniya ya Baqiyatullah (as) katika mji wa Zaria nchini Nigeria.
2012 Jul 16 , 23:43
Wazungumzaji waliopewa fursa ya kuzunguza katika sherehe za nusu Shaaban zilizoandaliwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Paris Ufaransa walijadili suala la mwanadamu mkamilifu kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu
2012 Jul 11 , 16:59
Sheikh Hussein bin Abdullah Rajab, muadhini wa Msikiti wa Mtume (saw) mjini Madina aliaga dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 85.
2012 Jul 09 , 13:02