IQNA

Vikosi vya Saudia vyashambulia nyumba za watu mjini Awamiya

13:05 - January 12, 2015
Habari ID: 2699769
Vikosi vya usalama nchini Saudi Arabia vimezishambulia nyumba kadhaa za jamii ya Waislamu wa Kishia katika mji wa Awamiya katika mkoa wa Qatif wakati huu ambapo utawala wa Saudi Arabia umezidisha vitendo vyake vya ukandamizaji dhidi ya wapinzani nchini humo.

Wanachama wa harakati ya Free Youth Movement (Harakat Shabab al Ahrar) wameripoti kujiri mashambulizi hayo kupitia ujumbe uliotumwa na harakati hiyo hii leo katika ukurasa wa facebook. Vikosi vya utawala wa Saudi Arabia vimezingira nyumba za raia katika vitongoji kadhaa vya mji wa Awamiya unaokaliwa na Waislamu wa Kishia ambapo pia sauti za ufyatuaji risasi zimesikika. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu watu waliouliwa au kujeruhiwa na vikosi vya usalama vya Saudi Arabia katika mashambulizi hayo. Itakumbukwa kuwa, tarehe 20 Disemba mwaka jana watu wasiopungua watano waliuliwa na vikosi vya Saudia katika mji wa Awamiya na wengine kadhaa kujeruhiwa. Wahanga wa mauaji hayo walikuwa ni wanaharakati wanaopigania demokrasia na wanaoupinga utawala ulioko madarakani wa ukoo wa Aal Saudi, huko Saudi Arabia.../mh

2696400

captcha